Kuchunguza Mchomozo Katika Fasihi ya Kiswahili: Utafiti Linganishi wa Ushairi Katika Diwani ya Ustadhi Andanenga

Tendwa, John Augustino (2017) Kuchunguza Mchomozo Katika Fasihi ya Kiswahili: Utafiti Linganishi wa Ushairi Katika Diwani ya Ustadhi Andanenga. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TENDWA_-TASNIFU-24-01-2017.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (568kB) | Preview

Abstract

Lengo la utafiti huu kama lilivyobainishwa katika sura ya kwanza ilikuwa ni kuchunguza Mchomozo katikaDiwani ya Ustadh Andanenga ili kubaini vipengele vya Mchomozovilivyotumika katika kufikisha ujumbe kwa jamii. Utafiti huu ulitumia mbinu moja ya ukusanyaji data ambayo ni; maktaba.Aidha data za utafiti huu zilichambuliwa kwa kutumia mbinu ya uchambuzi linganishi. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Karl Maks katika Uchambuzi wa Matini za Kifasihi. Utafiti umegundua kuwa, Diwani ya Ustadh Andanenga imetumia vipengele vya mchomozo ambavyo ni takriri na ukengeushi .Aidha utafiti huu umebaini kuwa, kipengele cha takriri silabi / mizani ndicho kimejitokza zaidi. Utafiti huu umebaini kuwa diwani hii iliandikwa katika cha mwaka 1990, msanii akiwataka wananchi kufanya kazi na kujitegemea ili kuepuka kutegemea misaada kwa Wazungu. Diwani inawataka watu waishi kwa kupendana , wathamini lugha ya Kiswahili kwani huo ni ukombozi wa kifikra endapo tutathamini utamaduni wetu.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 30 Mar 2017 07:45
Last Modified: 23 May 2017 08:48
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/1844

Actions (login required)

View Item View Item