Kutathmini Mila na Desturi za Mwanamke wa Visiwani katika Tenzi za Howani na Mwana Kukuwa

Mohamed, Fatma Ali (2016) Kutathmini Mila na Desturi za Mwanamke wa Visiwani katika Tenzi za Howani na Mwana Kukuwa. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of UTAFITI_-_FKM_FINAL-_HABIBA.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (724kB) | Preview

Abstract

Diwani ya Howani Mwana Howani ni Diwani ambayo imekusanya tenzi mbili ambazo ni Howani na Mwana Kukuwa.Tenzi hizo zinazungumzia mila na desturi za Mwanamke wa Visiwani kuanzia alipobeba ujauzito mpaka alipoolewa na kupelekwa kwake. Hivyo katika utafiti huu mtafiti alichunguza vipengele vya fani kama vile: matumizi ya lugha, mandhari na wahusika ili kuona ni jinsi gani mila na desturi za mwanamke wa visiwani zilivyojidhihirisha katika tenzi teule. Utafiti huu ulitumia mbinu ya maktabani. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya usomaji makini na upitiaji wa nyaraka. Wateuliwa wa utafiti huu waliteuliwa kwa kutumia mbinu ya uteuzi lengwa. Aidha, data zilizokusanywa katika utafiti huu, zilichambuliwa kwa kutumia mbinu ya kimaelezo. Utafiti huu umegunduwa kuwa tenzi za Howani na Mwana Kukuwa zimejedili kwa kiasi kikubwa mila na desturi za mwanamke wa visiwani. Mila na desturi hizo zimeanzia tokea mwanamke alipokuwa mja mzito, kipindi cha kujifunguwa, malezi ya mtoto wa kike, kipindi cha kubaleghe, kipindi cha ndoa, katika mavazi, mapambo, ngoma za asili, pamoja na tiba za asili. Utafiti huu umeongozwa na Nadharia ya Sosholojia katika kuelezea lengo mahsusi la kwanza na la pili na Nadharia ya Semiotiki imetumika katika kuchambua data zinazohusiana na lengo mahsusi la tatu, ili kufikia lengo la utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa vipengele kama vile mandhari, matumizi ya lugha pamoja na wahusika vimejitokeza kwa kiasi kikubwa katika tenzi za Howani na Mwana Kukuwa, vipengele hivyo vimesaidia sana katika kufikisha malengo ya Mwandishi ya kuelezea Mila na Desturi za mwanamke katika jamii ya visiwani Zanzibar.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 30 Mar 2017 07:41
Last Modified: 23 May 2017 09:05
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/1841

Actions (login required)

View Item View Item