Kuchunguza Dhima za Nyimbo za Ngoma ya Kibati Mkowa wa Kusini Pemba

Rashid, Halima Saleh (2016) Kuchunguza Dhima za Nyimbo za Ngoma ya Kibati Mkowa wa Kusini Pemba. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of UTAFITI_-_HALIMA_SALEH_RASHID_-_FINAL.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (600kB) | Preview

Abstract

Nyimbo za ngoma ya Kibati ni nyimbo maarufu sana visiwani Zanzibar. Asili ya nyimbo hizo ni kutoka kisiwani Pemba, katika Mkoa wa Kusini, Wilaya ya Mkoani katika kiambo cha Chokocho Michenzani. Nyimbo hizo zimekuwa maarufu sana na zinaendelea kupendwa kutwa kucha. Utafiti huu umefanywa, kuchunguza dhima zinazopatikana katika nyimbo hizo. Data zilichambuliwa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo na wa kidhamira. Nadharia ya dhima na kazi na Nadhariaya simiotiki, zilitumika katika kutimiza lengo la utafiti huu. Matokeo ya utafiti yameonyesha kwamba, dhima zinazojitokeza katika nyimbo za ngoma ya Kibati zimeweza kuakisi hali halisi ya maisha ya Wazanzibari katika Nyanja zote za maisha Kisiaasa, kiutamaduni, Kiuchumi na Kijamii. Aidha matokeo ya utafiti yameaonesha kwamba, mbinu za kisanaa zilizotumiwa na watunzi wa nyimbo za ngoma ya Kibati zimesheheni mafumbo, taswira, semi pamoja na matumizi ya lugha ya ishara. Kwa mfano wimbo wa Samaki wa Pono, utamu wa Ndizi, Mkate wa Mayai, Danganyayo zote zimejaa matumuzi ya taswira, semi, ishara na mafumbo.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 30 Mar 2017 07:43
Last Modified: 23 May 2017 08:55
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/1840

Actions (login required)

View Item View Item