khamis, Wahida Ameir
(2016)
Kuchunguza Dhamira za Nyimbo za Siti Bint Saad.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Utafiti huu umeshughulikia dhamira za nyimbo za Siti binti Saad. Ili kukamilisha lengo kuu, madhumuni mahususi mawili yalitimizwa. Madhumuni hayo yalihusu kuchunguza na kutathminidhamira za nyimbo za Siti binti Saad na kubainisha mbinu za kisanii zilizotumiwa na msanii huyo katika kuibua dhamira. Mtafiti ametumia mbinu za uchambuzi wa kifasihi, usaili katika kukusanya data za utafiti. Mikabala ya kimaelezo na ule wakifasihi ndiyo iliyotumika katika kuchambua data za utafiti wetu.Kwa jumla, utafiti umeweza kukusanya data ambazo zimeweza kujibu maswali yaliyoulizwa kutokana na madhumuni mahsusi yautafiti huu ambapo imedhihirika kwamba, nyimbo za Siti binti Saad zimeshehenidhamira za matabaka utamaduni na mapenzi.Pia imebainika kwamba mbinu za kisanaa zimetumika kujenga dhamira, miongoni mwa dhamira zilizoibuliwa nimatabaka utamaduni na mapenzi. Mbinu za kisaniizilizotumika ni kama mbinu ya simulizi, takriri, tashbiha, tash-hisi, ishara, misemo na muingiliano wa tanzu. Mwishoni mwa utafiti, kumetolewa mapendekezo kwa ajili ya tafiti zijazobaadae katika uwanja wa nyimbo za Siti binti Saad katika vipengele vyengine vya fani na maudhui kama vile matumizi ya lugha kwa upana zaidi, muundo, falsafa, ujumbe na maadili, mtazamo na msimamo.
Actions (login required)
|
View Item |