Kutathimini Mbinu za Ufutuhi Katika Kuelimisha Jamii Kuhusu Janga la Ukimwi,Katika Tamthiliya ya Embe Dodo Ushuhuda wa Mifupa

Gwanko, Lucy Chakupewa (2017) Kutathimini Mbinu za Ufutuhi Katika Kuelimisha Jamii Kuhusu Janga la Ukimwi,Katika Tamthiliya ya Embe Dodo Ushuhuda wa Mifupa. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of Lucy_Chakupewa-Mbinu_za_ufutuhi-03-06-2016-1_mpya.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (421kB) | Preview

Abstract

Lengo la utafiti huu ni kuchunguza mbinu za ufutuhi katika kufikisha maudhui katika tamthiliya kwa kulinganisha kazi mbili za tamthiliya ya Embe dodo na Ushuhuda wa Mifupa ili kubaini mbinu za ufutuhi zinavyowafananisha na kuwatofautisha wasanii wa vitabu hivyo katika kuliwasilisha suala la ugonjwa wa ukimwi na njia za kuenea kwa ugonjwa wa ukimwi. Utafiti huu ulitumia mbinu moja ya ukusanyaji data ambazo ni; maktaba. Aidha data za utafiti huu zilichambuliwa kwa kutumia mbinu ya uchambuzi linganishi. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Elimumitindo katika Uchambuzi wa Matini za Kifasihi. Utafiti umegundua kuwa, tamthiliya hizi zinatofautiana katika mbinu za kisanii na ubunifu. Tamthiliya ya Embe dodo imetumia mbinu za ufutuhi ubeuzi zaidi wakati tamthiliya ya Ushuhuda wa Mifupa imetumia mbinu ya ufutuhi uzimbwe zaidi, rahisi na ya wazi zaidi. Aidha utafiti huu umebaini kuwa, tamthiliya hizi zinatofutiana katika kuwasilisha suala la ugonjwa wa ukimwi na njia za kuenea kwake katika jamii ya Tanzania katika vipindi viwili tofauti. Embe dodo anawasilisha suala la mila na desturi linavyopingana na njia za kujikinga na ugonjwa wa ukimwi wakati Ushuhuda wa Mifupa inajadili kwa uhalisia juu ya njia mbali mbali ambazo zilisababisha zaidi kuenea kwa ugonjwa wa ukimwi, ambazo ni ujinga, umaskini na jamii kutokujali. Kwa upande mwingine, ilibainika kuwa tamthiliya hizi kwa vile zimeandikwa na wasanii wa jamii moja ambao wameshuhudia na kupata kuona na masimulizi ya historia ya jamii yao juu za ugonjwa wa ukimwi. Wasanii hawa wanafanana katika kuwasilisha maudhui ya kazi zao ambapo wote kwa pamoja wanajadili juu ya mambo mbalimbali yaliyopo katika jamii kama vile; rushwa, harakati za ukombozi, usaliti, mfumo dume, nafasi ya mwanamke, suala la ugonjwa wa ukimwi.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 01 Mar 2017 08:03
Last Modified: 23 May 2017 10:41
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/1754

Actions (login required)

View Item View Item