Ali, Jalghm Abuazoum Emhemmd
(2017)
Kuchunguza Dhamira katika Riwaya ya Kiu ya Mohamed Suleiman Mohamed.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Mada ya utafiti huu ilikuwa ni Kuchunguza Dhamira katika riwaya ya Kiu ya Mohamed Suleiman Mohamed. Mada hii iliundwa na lengo kuu na malengo mahususi. Lengo kuu la utafiti lilikuwa ni kuchunguza dhamira za kijamii katika riwaya ya Kiu ya Mohamed Suleiman. Malengo mahususi ya utafiti yalikuwa ni kuchambua dhamira za kijamii zinazowasilishwa katika riwaya ya Kiu ya Mohamed Suleiman na kuelezea mbinu za kifani zilizotumika katika kuwasilisha dhamira za kijamii katika riwaya ya Kiu ya Mohamed Suleiman.Data za msingi za utafiti huu zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya usomaji makini na ile upitiaji wa nyaraka ikitumika katika kukusanya data za upili. Data za utafiti zilichambuliwa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo na nadharia ya Sosholojia. Kimsingi, matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa dhamira za kijamii zinazojitokeza katika riwaya ya Kiu ni usafi wa mazingira, mapenzi katika jamii, wizi na magendo, umaskini na ujasiriamali. Dhamira hizi zimewasilishwa katika riwaya ya Kiu kwa kutumia mbinu za kifani za matumizi ya barua, misemo, sitiari, tashihisi na taharuki.
Actions (login required)
|
View Item |