Abdulla, Halima Salim
(2016)
Viambishi njeo katika vitenzi vya lahaja ya Kipemba : Uchanganuzi wa kimofofonolojia kuonesha muundo ndani na muundo nje.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Kazi hii inachambua mofofonolojia ya vitenzi vya lahaja ya Kipemba kuonesha muundo ndani na muundo nje . Utafiti ulilenga ubainisha mambo matatu; kwanza kuchunguza viambishi njeo katika vitenzi vya lahaja ya Kipemba; pili kueleza
michakato ya kimofofonolojia inayojitokeza katika kubadilisha miundo ndani na miundo nje; na tatu kudhihirisha kanuni zinazotawala mabadiliko ya muundo ndani na muundo nje katika vitenzi vya lahaja ya Kipemba. Utafiti huu ulifanyika katika Shehia ya Mtambwe Kaskazini katika jimbo la Mtambwe ambalo lilihusisha kijiji cha Kele, Uondwe, Mpakanjia, Jambaji, Kiapaka na Chanjaani. Watoa taarifa za utafiti walikuwa wakaazi asilia wa Mtambwe Kaskazini wenye umri kati ya miaka sitini nakuendelea ambao waliteuliwa kumi kutoka kila kijiji kwa njia ya usampulishaji bahati nasibu. Mbinu mbalimbali za utafiti zilitumika katika utafiti huu zikiwemo mbinu ya dodoso, usaili na uchunguzi makini. Matokeo ya utafiti yameonyesha michakato ya kimofofonolojia inavyojitokeza kwenye mabadiliko kutoka muundo ndani kwenda muundo nje katika vitenzi vya lahaja ya Kipemba na
kubainisha kanuni zinazotawala mabadiliko yanayotokea kutoka muundo ndani kwenda muundo nje katika vitenzi vya lahaja za Kipemba.
Actions (login required)
|
View Item |