Fakih, Sharif Juma
(2017)
Kutathmini mabadiliko ya usawiri wa mwanamke katika riwaya ya Utengano na Kamwe si mbali tena: Utafiti linganishi.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Utafiti huu unahusu Kutathmini Mabadiliko ya Usawiri wa Mwanamke katika riwaya za Utengano na Kamwe si mbali tena: Utafiti linganishi.Utafiti huu ni utafiti linganishi ambao lengo kuu ni Kutathmini kwa undani ni kwa vipi mwandishi
amekuwa na amebadilika katika kumsawiri mwanamke kupitia riwaya hizi mbili teule ikizingatiwa riwaya hizi zimepishana kwa miaka thelathini na nne (34). Riwaya ya Utengano ni katika riwaya za mwanzo (1980) na riwaya ya Kamwe si mbali tena ni katika riwaya mpya (2014) za mwandishi Said Ahmed Mohamed. Katika kufikia malengo ya utafiti huu, mtafiti alitumia nadharia ya Ufeministi wa Kiafrika kwa
lengo la kumsawiri mwanamke na alitumia nadharia ya Fasihi linganishi kwa lengo la kutathmini kufanana na kutofautiana kwa usawiri huo wa mwanamke katikariwaya hizi mbili teule za Utengano na Kamwe si mbali tena. Mtafiti alibaini kuwa riwaya hizi zimetafautiana katika kumsawiri mwanamke na hii ni kutokana na mabadiliko ya wakati, mazingira, utamaduni na mahitajio ya mwanadamu ingawaje yako yanayofanana. Mfano katika usawiri wa mwanamke yanayolingana ni pamoja na mwanamke kama muhusika mwenye mapenzi ya dhati, daktari wa kienyeji, msimamo thabiti, muwajibikaji na mlezi wa familiya. Kwa upande wa kutofauti ana,katika riwaya ya Utengano mwanamke amesawiriwa kama: Mshauri mwema, jasiri
na mwenye kujitoa mhanga, mlevi, mwenye mipango na hadaa na mtenda rushwa. Katika riwaya ya Kamwe si mbali tena mwanamke amesawiriwa kama: Msomi, mpenda dini, msamehevu, yatima, mwenye huruma na imani thabiti, mwenye tamaa, jeuri na kiburi.Hali hii imedhihirisha kuwa, tabia njema ndizo zinazostahili kufuatwa na zile mbaya ndizo za kuachwa na ndio siri ya mafanikio.
Actions (login required)
|
View Item |