Kuchunguza Dhamira za Nyimbo za Uganga Katika Jamii za Waswahili Wilaya ya Mkoani Kusini Pemba

Ali, Mussa Yussuf (2016) Kuchunguza Dhamira za Nyimbo za Uganga Katika Jamii za Waswahili Wilaya ya Mkoani Kusini Pemba. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of UTAFITI_-_MUSSA_YUSUF_ALI_-FINAL.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (676kB) | Preview

Abstract

Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza dhamira za nyimbo za Uganga katika jammi za waswahili Wilaya ya Mkoani Kusini Pemba. Ili kutimiza lengo hili kuu tulikuwa na madhumuni mahususi matatu ambayo ni kubainisha dhamira zinazopatikana katika nyimbo za uganga, kufafanua undani wa dhamira za nyimbo za uganga zilimo katika jamii ya watu wa Kusini Pemba na kufafanua vipengele vya kifani vinavyosaidia kuibua dhamira zinazojitokeza katika nyimbo za uganga. Data za utafiti zimekusanywa kwa kutumia njia ya usaili na njia shirikishi katika maskanini. Data hizo zilikusanywa na kuchambuliwa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo. Vile vile njia za kimaktaba zilitumika kwa mtafiti kwa ajili ya kujisomea kazi tangulizi na maandiko tafauti kwa lengo la kujiongezea maarifa na kufanikisha utafiti wake. Pia uchambuzi wa data ulifanywa kwa kutumia mkabala wa kinadharia. Nadharia zilizotumika ni Simiotiki na Mwitiko wa Msomaji. Ama kuhusu matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa kwenye nyimbo za uganga kuna siri ambazo zimejificha na zilihitajika kuwekwa bayana na mtafiti. Kwa upande wa dhamira zilizojitokeza katika nyimbo za uganga zilitoa dhamira kama vile suala la Mmongonyoko wa Maadili, umoja na mshikamano, malezi, matabaka na kadhalika. Mwisho matfiti alitoa hitimisho, mapendekezo ya tafiti nyingine zifanyika katika muktadha wa uganga kwa kuangalia misamiati na njungu katika tiba ya uganga na kuiomba jamii yake iziendeleze tiba za asili katika fani ya uganga.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 16 Feb 2017 09:51
Last Modified: 17 Oct 2018 13:12
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/1621

Actions (login required)

View Item View Item