Anusa, Anaphy Chiumbo
(2016)
Maana za Majina ya Watu katika Jamii ya Wayao.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Utafiti huu ulilenga kuchunguza majina ya watu katika jamii ya Wayao ili kuona iwapo yana maana. Kulikuwa na haja ya kufanyika utafiti huu ili kutoa mchango wa kitaaluma katika semantiki kuhusu maana za majina ya watu katika jamii hii. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya semiotiki ili kuweza kutimiza malengo ya utafiti huu na pia kujibu maswali ya utafiti huu. Data za utafiti huu zilikusanywa kwa kutumia njia ya usaili, hojaji[dodoso] na maktabani. Eneo la utafiti lilikuwa wilaya ya Tunduru nchini Tanzania katika vijiji vya Kidodoma,Nampungu na Nandembo.Walengwa wa utafiti huu walikuwa Wayao wote wanaojua maana za majina ya watu yenye asili ya Kiyao.Jumla ya watafitiwa 30 walishiriki katika utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yamedhihirisha kuwa majina ya watu katika jamii ya Wayao yana maana.Ni dhahiri kuwa utafiti huu utatoa mchango mkubwa katika taaluma ya Semantiki na katika tafiti za lugha za kibantu,na kuwa kichocheo cha kufanywa tafiti nyingine kuhusiana na mada hii na kuhusiana na jamii hii.
Actions (login required)
|
View Item |