Bwanga, Mwanamvua Mfamau
(2016)
Usawiri wa Mama wa Kambo Ndani ya Ngano za Kiswahili za Zanzibar katika Kipengele cha Malezi.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Kuna dhana iliyozoweleka katika ngano na katika maisha yetu ya kila siku, sio tu ndani ya jamii ya Zanzibar bali katika sehemu nyingi duniani, kuwa Mama wa Kambo ni wakatili, waovu, watesaji na hata wauaji wa watoto wanaowalea. Ni dhana hiyo ndiyo iliyotushawishi kutafuta ukweli. Jee!, katika uhalisia ni kweli Mama wa Kambo ni waovu kama walivyo katika ngano? Ili kupata ukweli huo, tulikusanya Ngano kutoka sehemu mbalimbali za Visiwa vya Unguja na Pemba. Baada ya kuzisoma zote, hakuna hata moja iliyomuonesha Mama wa Kambo kuwa ni mtu mwema. Ndipo tulipoamua kwenda katika jamii ili kuihoji inamuonaje Mama wa Kambo. Katika jamii, tulifanya majadiliano na wanafunzi 90, wakiwemo wana wa kambo na wanaolelewa na wazazi wao au wengine. Ni wanafunzi 11 tu walimtetea Mama wa Kambo, lakini 79 walimwelelezea kama ni muovu. Baadaye tuliyahoji makundi manne: Watoto wanaolelewa na Mama wa Kambo, Watu wazima waliowahi kulelewa na Mama wa Kambo, Mama wa Kambo wenyewe na Majirani waliokuwa wanawaelewa watoto wa kambo. Kwenye kundi la kwanza, hakuna hata mmoja aliyesema moja kwa moja kuwa Mama wa Kambo ni wazuri bali walikiri kuwa wapo Wazuri na Wabaya. Hii ni tafauti na kundi la pili ambapo wote walikiri kuwa walipata malezi mazuri kutoka kwa mama zao wa kambo. Ama Mama wa Kambo wenyewe, hakuna hata mmoja aliyekiri kuwa yeye ni muovu, ingawaje walidai kuwajua walio waovu. Na kundi la mwisho, lilidai kuwa wapo Mama wa Kambo wabaya, lakini na wazuri wapo. Kwa hivyo, kutokana na data na maelezo tuliyokusanya, utafiti umegundua kuwa katika ngano, Mama wa Kambo wote ni wabaya lakini katika uhalisa wapo Mama wa Kambo wabaya na wazuri.
Actions (login required)
|
View Item |