Magesa, January Peter Nyawema ,
(2017)
Ulinganishi Changanuzi wa Mofu Njeo za Kikara na Kiswahili.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Lengo la utafiti huu lilikuwa kuchunguza, kubaini na kulinganisha mofu njeo za kitenzi cha Kikara na za Kiswahili ili kujua idadi yake, mazingira zinapotokea na athari ya maumbo yake inayotokana na mazingira zilimo. Utafiti huu ulifanywa katika kata za Bukiko na Nyamanga wilaya ya Ukerewe kwa kuwatumia watoa habari 45 waliosailiwa na kujibu maswali. Utafiti huu umetumia nadharia ya Ulalo ya Reichenbach ambayo huchunguza, hubainisha na kulinganisha mofu njeo katika lugha ya Kikara na Kiswahili. Aidha nadharia hii inahusisha maumbo ya mofu njeo kwa kuonyesha wakati uliopita, wakati uliopo na wakati ujao. Mbinu ya utafiti iliyotumika katika kukusanya data ilikuwa ni usaili na dodoso. Katika utafiti huu watoa taarifa waliteuliwa kwa kuzigatia kigezo cha usampulishaji lengwa na nasibu. Uchambuzi wa data ulibainisha kuwa lugha zilizochunguzwa zilikuwa na idadi tofauti ya mofu njeo. Kikara kina jumla ya mofu njeo saba ilihali Kiswahili kina mofu njeo tano. Utafiti huu uligundua mazingira ya kutokea kwa mofu njeo hizi katika vitenzi yalikuwa tofauti kwa baadhi ya mofu njeo na kufanana kwa mofu nyingine. Aidha maumbo ya mofu katika vitenzi yaliathiriwa na mazingira yalimokuwa, ambazo husababishwa na muungano wa irabu zinazokabiliana katika kingo zake.
Actions (login required)
|
View Item |