Changamoto za Kutumia Istilahi Mbili kwa Dhana Moja Katika Kufundisha Isimu na Fasihi Shule za Sekondari: Mfano Kutoka Mkoa wa Kusini Pemba, Tanzania

Abdalla, Saleh Ali (2016) Changamoto za Kutumia Istilahi Mbili kwa Dhana Moja Katika Kufundisha Isimu na Fasihi Shule za Sekondari: Mfano Kutoka Mkoa wa Kusini Pemba, Tanzania. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of Saleh_Abdallah-TASNIFU-MA_Kiswahili_-10-10-2016.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (844kB) | Preview

Abstract

Utafiti huu umeshughulikia changamoto za kutumia istilahi mbili kwa dhana moja katika kufundisha isimu na fasihi shule za sekondari za Tanzania. Lengo la utafiti huu ni kuchunguza matumizi ya istilahi mbili kwa dhana moja katika kufundisha isimu na fasihi ya Kiswahili kwa shule za sekondari, kudadisi usuli wake na kupendekeza njia za kuondokana na tatizo hili. Utafiti huu umetumia muundo wa kimaelezo na mbinu ya usampulishaji iliyotumika ni usampulishaji nasibu tabakishi na umefanywa katika baadhi ya shule za mkoa wa kusini Pemba. Mbinu zilizotumika kukusanya data ni mbinu ya dodoso. Kuhusu matokeo ya utafiti imebainika kwamba kuna matumizi makubwa ya istilahi mbili kwa dhana katika shule za sekondari katika kufundisha isimu na fasihi ya Kiswahili. Hali hii imesababisha wanafunzi kukanganyikiwa, kufeli na hata kulichukia somo. Kwa hivyo matumizi ya istilahi mbili kwa dhana moja ni dhahiri kuwa huathiri ujifunzaji wa isimu na fasihi ya Kiswahili. Mapendekezo yanayotokana na utafiti huu ni pamoja na kuanzisha vitengo vya kuunda na kusimamia matumizi ya istilahi kwa ujumla.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 14 Feb 2017 12:35
Last Modified: 22 Oct 2018 09:43
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/1605

Actions (login required)

View Item View Item