Abdalla, Saleh Ali
(2016)
Changamoto za Kutumia Istilahi Mbili kwa Dhana Moja Katika Kufundisha Isimu na Fasihi Shule za Sekondari: Mfano Kutoka Mkoa wa Kusini Pemba, Tanzania.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Utafiti huu umeshughulikia changamoto za kutumia istilahi mbili kwa dhana moja katika kufundisha isimu na fasihi shule za sekondari za Tanzania. Lengo la utafiti huu ni kuchunguza matumizi ya istilahi mbili kwa dhana moja katika kufundisha isimu na fasihi ya Kiswahili kwa shule za sekondari, kudadisi usuli wake na kupendekeza njia za kuondokana na tatizo hili. Utafiti huu umetumia muundo wa kimaelezo na mbinu ya usampulishaji iliyotumika ni usampulishaji nasibu tabakishi na umefanywa katika baadhi ya shule za mkoa wa kusini Pemba. Mbinu zilizotumika kukusanya data ni mbinu ya dodoso. Kuhusu matokeo ya utafiti imebainika kwamba kuna matumizi makubwa ya istilahi mbili kwa dhana katika shule za sekondari katika kufundisha isimu na fasihi ya Kiswahili. Hali hii imesababisha wanafunzi kukanganyikiwa, kufeli na hata kulichukia somo. Kwa hivyo matumizi ya istilahi mbili kwa dhana moja ni dhahiri kuwa huathiri ujifunzaji wa isimu na fasihi ya Kiswahili. Mapendekezo yanayotokana na utafiti huu ni pamoja na kuanzisha vitengo vya kuunda na kusimamia matumizi ya istilahi kwa ujumla.
Actions (login required)
|
View Item |