Athari za Kiisimu za Lahaja ya Kitumbatu katika Kiswahili Sanifu Kinachotumika katika Shule za Tumbatu Zanzibar

Ame, Pandu Machano (2017) Athari za Kiisimu za Lahaja ya Kitumbatu katika Kiswahili Sanifu Kinachotumika katika Shule za Tumbatu Zanzibar. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of MW._PANDU__(UTAFITI_2)_-_HABIBA.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (898kB) | Preview

Abstract

Utafiti huuumejadili “Athari za Kiisimu za Lahaja za Kitumbatu katika Kiswahili Sanifu Kinachotumika Katika Shule za Tumbatu Zanzibar”.Utafiti ulifanyika Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja na uliongozwa na Nadharia Kidhi ya Mawasiliano. Nadharia hiyo ilianzishwa na Howard (1973) ambayo lengo lake kuu ni kueleza sababu za kubadili mtindo wa matamshi wakati wa mawasiliano wa kijamii na kuangalia athari zake katika jamii. Katika utafiti huu, data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya hojaji, usaili na uchunguzi shirikishi. Jumla ya watafitiwa walikuwa 68. Miongoni mwao walimu walikuwa 29, na wanafunzi walikuwa 39. Vilevile utafiti huu umeonesha matokeo. Miongoni mwa matokeo hayo ni kwamba lahaja ya Kitumbatu baadhi ya wakati maumbo ya maneno hutumia ulahaja. Pia, lahaja ya Kitumbatu hudondosha viambishi katika maneno.Mwisho, sura imehitimisha kwa kutoa mapendekezo ambayo yatasaidia wanajamii kufanya tafiti kwa za lahaja mbalimbali kwa lengo la kuweka kumbukumbu kwa vizazi vya baadaye.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 14 Feb 2017 12:36
Last Modified: 23 May 2017 12:00
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/1595

Actions (login required)

View Item View Item