Ujidhihirishaji wa Mofu Nafsi na Njeo Katika Kiswahili: Utafiti Linganishi wa Lahaja ya Kipemba na Kiswahili Sanifu

Hassan, Hafsa Sadra (2016) Ujidhihirishaji wa Mofu Nafsi na Njeo Katika Kiswahili: Utafiti Linganishi wa Lahaja ya Kipemba na Kiswahili Sanifu. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of HAFSA-_FINAL_latest.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (354kB) | Preview

Abstract

Kazi hii ilihusika na Ujidhihirishaji wa Mofu zinazowakilisha Nafsi na Njeo Katika Kiswahili: Utafiti linganishi wa lahaja ya Kipemba na Kiswahili sanifu. Utafiti huu ulikuwa na malengo mawili ambayo ni kulinganisha ujidhihirishaji wa mofu nafsi na njeo baina ya Kiswahili sanifu na Kipemba pamoja na kuchunguza namna mabadiliko ya kimofofonolojia yanavyoathiri maumbo ya mofu nafsi na njeo baina ya Kiswahili sanifu na lahaja ya Kipemba. Ili kufikia lengo kuu lililokusudiwa mbinu mbalimbali za utafiti zilihusika, ambazo ni hojaji, mahojiano pamoja na mbinu shirikishi. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni nadharia ya Mofofonolojia. Sampuli iliyotumika ni watu sitini na tano kutoka Pemba. Kwa upande wa matokeo ya utafiti, yanabainisha kwamba, kunatofauti kubwa ya udhihirikaji wa mofu nafsi na njeo baina ya Kipemba na Kiswahili sanifu, tofauti ambayo ipo katika vipengele viwili kwanza idadi ya maumbo ya mofu nafsi katika lahaja ya Kipemba ni kubwa kuliko Kiswahili sanifu. Pili mwonekano wa maumbo ya mofu nafsi na njeo na jinsi ya utendaji kazi wake. Aidha utafiti umebaini kuwa kuna mabadiliko ya kimofofonolojia ambayo yanayoathiri maumbo ya mofu nafsi na njeo katika lahaja ya Kipemba. Mabadiliko hayo huathiri muundo wa msingi wa mofu hizo. Utafiti umependekeza mambo kadhaa ya kuyafanyia kazi. Kwanza utafiti wa mofolojia unaohusu ulinganifu wa ujidhihirishaji wa mofu katika lahaja za Kiswahili unahitajika. Pia tunapendekeza kuwa, uchunguzi juu ya mofolojia ya lahaja mbali mbali unahitajika ili tuweze kuziba pengo liliopo.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 16 Feb 2017 09:52
Last Modified: 23 May 2017 11:42
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/1579

Actions (login required)

View Item View Item