Kutathmini Mabadiliko ya Usawiri wa Mwanamke Katika Riwaya ya Utengano na Kamwe si Mbali tena: Utafiti Linganishi.

Fakih, Sharif Juma (2017) Kutathmini Mabadiliko ya Usawiri wa Mwanamke Katika Riwaya ya Utengano na Kamwe si Mbali tena: Utafiti Linganishi. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of Fakih_S_-_Tasnifu_-24-01-2017.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (880kB) | Preview

Abstract

Utafiti huu unahusu Kutathmini Mabadiliko ya Usawiri wa Mwanamke katika riwaya za Utengano na Kamwe si mbali tena: Utafiti linganishi. Utafiti huu ni utafiti linganishi ambao lengo kuu ni Kutathmini kwa undani ni kwa vipi mwandishi amekuwa na amebadilika katika kumsawiri mwanamke kupitia riwaya hizi mbili teule ikizingatiwa riwaya hizi zimepishana kwa miaka thelathini na nne (34). Riwaya ya Utengano ni katika riwaya za mwanzo (1980) na riwaya ya Kamwe si mbali tena ni katika riwaya mpya (2014) za mwandishi Said Ahmed Mohamed. Katika kufikia malengo ya utafiti huu, mtafiti alitumia nadharia ya Ufeministi wa Kiafrika kwa lengo la kumsawiri mwanamke na alitumia nadharia ya Fasihi linganishi kwa lengo la kutathmini kufanana na kutofautiana kwa usawiri huo wa mwanamke katika riwaya hizi mbili teule za Utengano na Kamwe si mbali tena. Mtafiti alibaini kuwa riwaya hizi zimetafautiana katika kumsawiri mwanamke na hii ni kutokana na mabadiliko ya wakati, mazingira, utamaduni na mahitajio ya mwanadamu ingawaje yako yanayofanana. Mfano katika usawiri wa mwanamke yanayolingana ni pamoja na mwanamke kama muhusika mwenye mapenzi ya dhati, daktari wa kienyeji, msimamo thabiti, muwajibikaji na mlezi wa familiya. Kwa upande wa kutofautiana, katika riwaya ya Utengano mwanamke amesawiriwa kama: Mshauri mwema, jasiri na mwenye kujitoa mhanga, mlevi, mwenye mipango na hadaa na mtenda rushwa. Katika riwaya ya Kamwe si mbali tena mwanamke amesawiriwa kama: Msomi, mpenda dini, msamehevu, yatima, mwenye huruma na imani thabiti, mwenye tamaa, jeuri na kiburi. Hali hii imedhihirisha kuwa, tabia njema ndizo zinazostahili kufuatwa na zile mbaya ndizo za kuachwa na ndio siri ya mafanikio.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 16 Feb 2017 09:52
Last Modified: 22 Oct 2018 09:38
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/1573

Actions (login required)

View Item View Item