Kuchunguza Dhima ya Methali za Jamii ya Wasimbiti wa Rorya Mkoani Mara.

Angela , Ghati Sylvester (2016) Kuchunguza Dhima ya Methali za Jamii ya Wasimbiti wa Rorya Mkoani Mara. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of ANGELA_GHATI_SYLVESTER_-TASNIFU-13-10-2016.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (629kB) | Preview

Abstract

Mada ya utafiti huu ilikuwa ni kuchunguza dhima ya methali za jamii ya Wasimbiti wa Rorya mkoani Mara. Ili kufanikisha mada hii utafiti ulikuwa na madhumuni mahususi matatu ambayo ni kubainisha dhima ya methali ya jamii ya Wasimbiti wa wilaya ya Rorya mkoani Mara, kuelezea uhalisia wa dhima za methali za jamii ya Wasimbiti kwa jamii ya leo na kubainisha mbinu za kisanaa zilizotumika kujenga dhima za methali za jamii ya Wasimbiti. Madhumuni haya matatu yamefanyiwa kazi na matokeo ya utafiti yamepatikana. Data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia mbinu za usaili na upitiaji wa nyaraka na kuchambuliwa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo na nadharia za Sosholojia na Simiotiki. Matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa methali za jamii ya Wasimbiti zina dhima za kuhamasisha jamii kuepuka tamaa , kuwa na subira, kuelimisha jamii juu ya maisha, kufanya kazi kwa juhudi na maarifa, kuhimiza umoja na mshikamano katika jamii na umuhimu wa malezi kwa vijana katika jamii. Pia, matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa methali za jamii ya Wasimbiti zinaundwa na mbinu za kisanaa za mafumbo, takriri, taswira na muundo. Mbinu hizi za kisanaa zimesaidia sana katika kuwasilisha dhima za methali za jamii ya Wasimbiti wanaoishi wilaya ya Rorya mkoani Mara.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 16 Feb 2017 09:56
Last Modified: 23 May 2017 11:12
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/1538

Actions (login required)

View Item View Item