Ulinganishi wa kiisimu kati ya lahaja ya Kipemba na Kitumbatu

Bakari, Bakari Kombo (2015) Ulinganishi wa kiisimu kati ya lahaja ya Kipemba na Kitumbatu. Masters thesis, The Open University Of Tanzania.

[thumbnail of TASNIFU_YA_MWISHO_WA_MWISHO.pdf]
Preview
PDF
Download (541kB) | Preview

Abstract

Kazi hii ilihusika na Ulinganishi wa Kiisimu uliopo baina ya lahaja ya Kipemba na Kitumbatu.Utafiti huu ulikuwa na malengo matatu ambayo ni kubainisha tofauti baina ya fonimu za Kipemba na Kitumbatu, kulinganisha na kutofautisha kanuni za kifonolojia na kimofofonolojia zinazotawala maumbo ya mofu zilizounda maneno ya Kipemba na Kitumbatu na kuainisha uwiano wa kimaana baina ya msamiati wa lahaja ya Kipemba na Kitumbatu. Ili kufikia lengo kuu lililokusudiwa mbinu mbalimbali za utafiti zilihusika, ambazo ni hojaji, mahojiano pamoja na ushuhudiaji. Nadharia mbili zilizoongoza utafiti huu ni nadharia ya fonolojia zalishi na nadharia ya lahaja na lahajia na Sampuli iliyotumika ni watu mia moja, hamsini kutoka Pemba na hamsini kutoka Tumbatu. Kwa upande wa matokeo ya utafiti, mtafiti aligundua kwamba, kifonolojia kuna utofauti mkubwa baina ya Kipemba na Kitumbatu, hasa kwenye idadi na aina za fonimu kwa upande mmoja na tofauti ya kimatumizi katika baadhi ya fonimu kwa upande wa pili. Pia imebainika kuwa, Kipemba na Kitumbatu kina tofauti kwenye baadhi ya viambishi nafsi za mtenda na mtendwa. Kanuni za Kifonolojia zinazobadilisha miundo ya ndani kuwa miundo ya nje ya maumbo ya vitenzi, nomino na hata baadhi ya vivumishi na viwakilishi zimetumika katika lahaja zote mbili, ingawa kitumbatu kimezidi kujikita kwenye matumizi ya kanuni nyingi zaidi kuliko Kipemba. Kipemba kimetofautiana na Kitumbatu kwenye msamiati mwingi hasa kwenye vitenzi na nomno. Lakini katika eneo hili Kipemba kipo karibu zaidi na Kiswahili Sanifu, wakati Kitumbatu kimejitenga mbali na Kiswahili Sanifu katika uwiano wa kimsamiati. Mtafiti amependekeza mambo kadha na kuwaagiza watafiti wajao wayatupie macho na kuyafanyia kazi. Miongoni mwa mapendekezo hayo ni pamoja na kufanya tafiti linganishi baina ya lahaja za Kiswahili, kufanya Ulinganishi wa Kiisimu baina ya Vipemba vizungumzwavyo ndani ya visiwa vidogo vidogo ndani ya Pemba.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 13 Jul 2016 10:02
Last Modified: 13 Jul 2016 10:02
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/1479

Actions (login required)

View Item View Item