Kuchunguza Ufasihi Simulizi unaojitokeza Ndani ya Hadithi za Kusadikika na Adili na Nduguze

Salim, Muhammed Ali (2015) Kuchunguza Ufasihi Simulizi unaojitokeza Ndani ya Hadithi za Kusadikika na Adili na Nduguze. Masters thesis, The Open University Of Tanzania.

[thumbnail of TASINIFU_YA_MOHAMED_SALIMU_mpya_1__-__New__FINAL.pdf]
Preview
PDF
Download (796kB) | Preview

Abstract

Lengo la utafiti huu ni kuchunguza Ufasihi Simulizi unaojitokeza katika hadithi za Adili na Nduguze na Kusadikika za Shaaban Robert. Ili kukamilisha lengo hili, utafiti ulikuwa na malengo mahususi matatu ambayo ni; kufafanua vipengele vya fasihi simulizi vinavyojitokeza ndani ya hadithi za Kusadikika na Adili na Nduguze, kujadili mbinu zilizotumika katika kuhifadhi ufasihi simulizi uliomo ndani ya kazi husika, na kuelezea dhamira zinazojitokeza ndani ya hadithi za Kusadikika na Adili na Nduguze. Data za utafiti huu zimekusanywa kwa kutumia mbinu za usomaji makini na upitiaji wa nyaraka maktabani. Mkabala wa kimaelezo sambamba na nadharia za Mwitiko wa Msomaji na Ujumi ndizo zilizotumika katika kuchambua data za utafiti.Matokeo ya utafiti yamebaini kuwa fani za fasihi simulizi kama vile methali, misemo, hadithi ndani ya hadithi, nyimbo na masimulizi zimejitokeza kwa kiasi kikubwa katika kazi teule za Shaaban Robert. Vile vile, matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa mbinu za kisanaa kama vile; muundo, mtindo, wahusika, mandhari na matumizi ya lugha zimetumika katika kuhifadhi ufasihi simulizi katika riwaya husika. Pia, matokeo ya utafiti yamegundua kuwa, katika kazi hizo kunajitokeza dhamira kama vile; umuhimu wa elimu, kilimo, uongozi bora, umuhimu wa sheria, mapenzi, choyo na husda, ndoa, malezi na kodi. Kwa ujumla, utafiti huu umegundua kuwa fasihi ni moja tu. Maandishi au Masimulizi ni namna za uwasilishaji wa fasihi ya Kiswahili na nyinginezo duniani. Aidha, utafiti umegundua kuwa, Fasihi ya Maandishi hutumia vipengele vile vile vya Fasihi ya Masimulizi ili kufikisha ujumbe kwa jamii. Hivyo, mpaka uliopo ni namna ya uwasilishaji wa kazi hizo

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 13 Jul 2016 10:02
Last Modified: 13 Jul 2016 10:02
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/1477

Actions (login required)

View Item View Item