Kuchunguza Dhana Zilizobebwa na Wahusika na Zinavyolandana na Majina yao: Uchunguzi katika Riwaya ya Kiu na Kiu ya Haki

Ali, Amour Rashid (2015) Kuchunguza Dhana Zilizobebwa na Wahusika na Zinavyolandana na Majina yao: Uchunguzi katika Riwaya ya Kiu na Kiu ya Haki. Masters thesis, The Open University Of Tanzania.

[thumbnail of Tasinifu_ya_Amour_Rashid_M.A_Kiswahili.pdf]
Preview
PDF
Download (587kB) | Preview

Abstract

Utafiti huu unahusu kuchunguza dhana zilizobebwa na wahusika na zinavyolandana na majina yao katika riwaya ya Kiu na Kiu ya Haki. Ili kufikia lengo, mtafiti alichunguza na kubainisha wahusika, pia alichunguza mlandano wa wahusika kupitia mbinu mbali mbali na alichambua dhamira mbali mbali zilizobebwa na wahusika hao na jinsi zinavyolandana na majina yao katika riwaya teuliwa. Utafiti huu ulitumia mbinu ya maktabani. Riwaya teuliwa ziliteuliwa kwa kutumia mbinu ya malengo maalumu. Aidha, data za utafiti huu zilikusanywa na kuchambuliwa kwa mbinu ya kimaelezo kutoka katika riwaya teuliwa. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya sosholojia na nadharia ya mwitiko wa msomaji. Utafiti huu uligundua kuwa, kazi hizo teuliwa zimetumia wahusika wakuu, wahusika wasaidizi na wahusika wajenzi. Pia, utafiti umegundua kuwa, waandishi wa riwaya hizo teuliwa wametumia mbinu mbali mbali za kuwasawiri wahusika na kuwafanya walandane na majina yao. Mbinu hizo ni pamoja na mbinu ya majazi au majina, kimaelezi, kidrama kuwatumia wahusika wengine, ulinganuzi na usambamba na uzungumzi nafsi wa ndani. Pia, utafiti umegundua kuwa, dhamira katika riwaya teuliwa zimelandana na majina ya wahusika. Dhamira hizo ni pamoja na umasikini, wizi na ujambazi, utamaduni, dhamira ya malezi, dhamira ya ujirani, dhamira ya mapenzi, umuhimu wa elimu, nakadhalika.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 13 Jul 2016 10:02
Last Modified: 13 Jul 2016 10:02
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/1475

Actions (login required)

View Item View Item