Kuchunguza Matumizi ya Lugha katika Riwaya ya Kiswahili: Uchunguzi Kifani wa Vipuli vya Figo na Siri za Maisha

Kimambo, Sidora Joseph (2015) Kuchunguza Matumizi ya Lugha katika Riwaya ya Kiswahili: Uchunguzi Kifani wa Vipuli vya Figo na Siri za Maisha. Masters thesis, The Open University Of Tanzania.

[thumbnail of Sidora__TASINIFU.pdf]
Preview
PDF
Download (607kB) | Preview

Abstract

Riwaya za Vipuli vya Figo na Siri za Maisha ni riwaya mpya, kwa maana ya riwaya za karibuni zenye kusheheni matukio ya kusisimua na kutoa mafunzo kwa yeyote aliyewahi ama atakayezisoma aidha kwa kujiburudisha au kujifunza. Ni kazi nzuri na za kuvutia za Profesa Emmanuel Mbogo. Utafiti huu ulifanywa kwa lengo la kuchunguza matumizi ya lugha katika riwaya hizi mbili na kuibua dhamira mbalimbali zilizojitokeza. Utafiti huu ulikuwa na malengo mahususi matatu ambayo ni, kuchambua matumizi ya lugha ya kitamathali katika riwaya za Vipuli vya Figo na Siri za Maisha, kuchambua matumizi ya lugha yasiyo ya kitamathali katika riwaya za Vipuli vya Figo na Siri za Maisha na kuwasilisha dhamira zinazojitokeza katika riwaya za Vipuli vya Figo na Siri za Maisha. Katika kutimiza malengo haya, tulikusanya data kwa kutumia mbinu za usomaji makini na upitiaji wa nyaraka maktabani na kufanya uchambuzi wa data kwa kutumia mbinu ya mkabala wa kimaelezo na nadharia ya Simiotiki. Maokeo ya utafiti yanaonyesha kwamba, matumizi ya lugha yaliyojitokeza katika riwaya za Vipuli vya Figo na Siri za Maisha ni tamathali za usemi na zisizo tamathali za usemi. Matumizi ya lugha ya kitamathali ni tashibiha, tashihisi, tafsida, sitiari, kejeli na dhihaka. Matumizi ya lugha yasiyokuwa ya kitamathali ni misemo, nahau, takriri, tanakali sauti na taharuki. Pamoja na matumizi haya ya lugha ya kitamathali na yasiyokuwa ya kitamathali pia kuna dhamira mbalimbali zimejitokeza katika riwaya tafitiwa. Dhamira hizo ni biashara haramu, umuhimu wa elimu katika jamii, Dhamira ya malezi katika jamii, hali ngumu ya maisha, siasa na uchumi na nafasi ya mwanamke katika jamii.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 13 Jul 2016 10:03
Last Modified: 13 Jul 2016 10:03
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/1471

Actions (login required)

View Item View Item