Tathmini ya mwingilianomatini katika utunzi wa Emmanuel Mbogo: Utafiti Linganishi wa Tamthiliya ya Ngoma ya Ng’wanamalundi na Fumo Liongo

Mningo,, Rehema Adam (2015) Tathmini ya mwingilianomatini katika utunzi wa Emmanuel Mbogo: Utafiti Linganishi wa Tamthiliya ya Ngoma ya Ng’wanamalundi na Fumo Liongo. Masters thesis, The Open University Of Tanzania.

[thumbnail of REHEMA_FINAL_TASNIFU_(MPYA)-1_(3).pdf]
Preview
PDF
Download (997kB) | Preview

Abstract

Utafiti huu unahusu Tathmini ya mwingilianomatini katika utunzi wa Emmanuel Mbogo: Utafiti linganishi wa tamthiliya ya Ngoma ya Ng’wanamalundi na Fumo Liongo. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kufanya tathmini ya mwingilianomatini katika utunzi wa Emmanuel Mbogo, kwa kulinganisha tamthiliya ya Ngoma ya Ng’wanamalundi (1988) na Fumo Liongo (2009), ili kubaini jinsi mtunzi huyo anavyofumbata mbinu ya mwingilianomatini katika kazi zake za fasihi, na namna mbinu hiyo inavyotumika kuibua dhamira za tamthiliya hizo. Sampuli ya utafiti huu iliteuliwa kwa kutumia mbinu ya uteuzi wa madhumuni maalum, wakati ambapo data zilikusanywa kwa kutumia mbinu tatu, ambazo ni mapitio ya maandiko, usaili na majadiliano ya vikundi. Uchambuzi wa data ulifanyika kwa kutumia mbinu ya uchambuzi maudhui. Aidha nadharia ya mwingilianomatini ilitumika kukusanya, kuchambua na kujadili data za utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa, mtunzi ameendelea kufumbata mbinu ya mwingilianomatini katika utunzi wake, pamoja na kuwa kazi hizo zina mpishano wa takribani muongo mmoja katika kutungwa kwake. Aidha, tamthiliya zote mbili ni matokeo ya athari za mapokeo simulizi ya Kiafrika, ambapo mtunzi ameathiriwa na mapokeo simulizi ya ngano za kabila la Wasukuma kama dafina ya utunzi wa tamthiliya ya Ngoma ya Ng’wanamalundi na mapokeo simulizi ya utendi wa “Fumo Liongo” kama dafina ya utunzi wa tamthiliya ya Fumo Liongo.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 13 Jul 2016 10:05
Last Modified: 13 Jul 2016 10:05
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/1453

Actions (login required)

View Item View Item