Athari za lugha ya Kijita katika kujifunza Kiswahili

Wenceslaus, Mashaka (2015) Athari za lugha ya Kijita katika kujifunza Kiswahili. Masters thesis, The Open University Of Tanzania.

[thumbnail of MASHAKA_WENCESLAUS-_dissertation.pdf]
Preview
PDF
Download (1MB) | Preview

Abstract

Lengo la Tasnifu hii ni kuchunguza Athari ya lugha ya Kijita Katika Kujifunza lugha Kiswahili Kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi, sababu za athari hizo na mbinu za kutatua athari hizo. Utafiti huu umefanywa Wilaya ya Musoma vijijini na Manispaa ya Musoma katika mkoa wa Mara. Kata mbili zilishirikishwa ambazo ni kata ya Suguti na Makoko. Shule za msingi za Suguti, Kusenyi, Buhare, Nyarigamba na Mtakuja zilichunguzwa ili kubaini athari za lugha ya Kijita katika kujifunza Kiswahili.Utafiti huu umetumia nadharia ya Fonolojia Zalishi Asilia ambayo huchunguza bayana athari hizo za lugha ya kwanza ( Kijita) katika kujifunza lugha ya Kiswahili. Aidha nadharia hii huchukulia kuwa makosa katika lugha ya pili ( Kiswahili) husababishwa na athari ya lugha ya kwanza. Utafiti huu ulitumia mbinu tatu za ukusanyaji data ambazo ni; hojaji, mahojiano, na majadiliano ya vikunndi. Sampuli ya utafiti huu iliteuliwa kwa kutumia mbinu ya; madhumuni maalumu, kimfumo na uteuzi wa nasibu takabishi. Matokeo ya utafiti huu umegundua kuwa, athari za matamshi zinazojitokeza kwa wanafunzi wanapojifunza lugha ya Kiswahili ni pamoja na udondoshaji wa sauti , kutumia sauti zinazokaribiana, na kuongeza viambishi visivyohitajika. Aidha utafiti huu umegundua sababu zinazotokana na athari hizi ni lugha mama na athari ya kimazingira. Utafiti huu uligundua mbinu za kutatua tatizo hili ni watoto wafundishwe Kiswahili wakiwa bado wadogo na wazazi wawe mfano bora kwa watoto wao katika kuzungumza Kiswahili na kuwapa zana malimbali za ujifunzaji kwa mfano kamusi na kadhalika. Matokeo ya utafiti huu yaliwasilishwa katika sura ya nne, yanaweza kutumiwa na Taasisi ya ukuzaji mitaala kutoa mapendekezo kwa wanaojifunza Kiswahili kwa kuwashirikisha wanafunzi kimazungumzo kwa lengo la kuinua kiwango cha umilisi wa lugha.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 13 Jul 2016 10:12
Last Modified: 13 Jul 2016 10:12
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/1417

Actions (login required)

View Item View Item