Changamoto na mbinu za kiisimu katika ufundishaji wa stadi ya mazungumzo kwa wanafunzi wa elimu ya awali

Ali, Laila Hemed (2015) Changamoto na mbinu za kiisimu katika ufundishaji wa stadi ya mazungumzo kwa wanafunzi wa elimu ya awali. Masters thesis, The Open University Of Tanzania.

[thumbnail of LAILA_HEMED_FINAL___-__FINAL.pdf]
Preview
PDF
Download (491kB) | Preview

Abstract

Lengo la kazi hii ilikuwa ni kuchunguza uhusiano uliopo baina ya ufundishaji wa stadi ya mazungumzo kwa wanafunzi wa shule za elimu ya awali kisiwani Pemba na kukwama kwao kupata maarifa ya stadi hiyo vya kutosha. Utafiti huu umefanywa katika wilaya ya Chake Chake, mkoa wa Kusini, Pemba. Washiriki wa utafiti walikuwa ni mratibu wa kituo cha walimu wa elimu ya awali, wakaguzi wa somo la Kiswahili kwa walimu wa elimu ya awali, walimu wakuu na walimu wa elimu ya awali. Matokeo ya utafiti yamebaini kuwa, walimu hawana ujuzi wa kutosha wa kutumia njia za ufundishaji wa stadi ya mazungumzo. Wanafunzi hawajifunzi lugha yao ipasavyo kupitia mazungumzo kutokana na walimu kukosa umahiri katika ufundishaji. Walimu hawatumii zana za kufundishia ipasavyo katika ufundishaji wa stadi ya mazungumzo, hii imewafanya wanafunzi hawa kutojifunza lugha ya mazungumzo kwa umakini. Upungufu wa mafunzo kwa walimu ambayo yangewezesha walimu kufundisha kwa ufanisi umedumaza ufundishaji wa stadi ya mazungumzo. Mapendekezo yaliyopendekezwa ni walimu wa shule za awali wa somo la Kiswahili kupatiwa mafunzo yanayohusu ufundishaji wa stadi ya mazungumzo, njia za kufundishia stadi hii pamoja matumizi bora ya zana za kufundishia ili wanafunzi waweze kumudu kufundisha stadi ya mazungumzo. Tafiti nyingine zifanyike katika maeneo mengine ya Zanzibar na Tanzania ili kukuza ufanisi katika ufundishaji wa stadi ya mazungumzo.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 13 Jul 2016 10:15
Last Modified: 13 Jul 2016 10:15
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/1402

Actions (login required)

View Item View Item