Salim, Amina Said
(2015)
Kuchunguza dhima za semi zilizoandikwa kwenye mikoba Kisiwani Pemba.
Masters thesis, The Open University Of Tanzania.
Abstract
Kazi hii ilihusika na mada inayohusiana na dhima za semi zilizoandikwa kwenye mikoba katika jamii ya Kipemba.Imechunguza semi zilizoandikwa kweye mikoba kisiwani Pemba zinawafunza nini wapemba. Yaani zinawasilisha ujumbe wa aina ipi kwao,ili kufikia lengo kuu la utafiti huu lililokusudiwa.Mbinu mbali mbali za utafiti zilitumika,mbinu hizo ni pamoja na hojaji,mahojiano pamoja na uchunguzi makini.Sampuli lengwa na sampuli eneo zilitumika,kuchagua watoa taarifa kwa vigezo vya kazi yangu yaani viwanda vya kuchapishia mikoba.Nadharia mbili za utafiti huu zilitumika nadharia ya Mwitiko wa Msomaji na Sosholojia. Kwa upande wa matokeo mtafiti amegundua kwamba semi zilizoandikwa kwenye mikoba zimejigawa katika maudhui mbalimbali kama vile maudhui ya kimapenzi, subra na uvumulivu,mila na tamaduni za jamii,dua na maombi kutoka kwa Mungu, fitna na majungu,umbea na udaku,pamoja na uchumi na uzalishaji mali. Kwenye lengo la pili mtafiti alichambua dhima za kila kipengele miongoni mwa vipengele alivovibainisha na hatimae kwenye lengo la tatu aliangazia mbinu za kisanaa na akagundua mbinu mbalimbali za kisanaa zilizojitokeza katika semi zake. Utafiti unaendeleza mbele hatua za utafiti lugha ya Kiswahili na lahaja zake ambapo kazi hii inatoa mawazo ya awali katika kuelezea dhima za semi zilizoandikwa kwenye mikoba kisiwani Pemba.
Actions (login required)
|
View Item |