Liwachi,, Vincent Stanley
(2015)
Nafasi ya Nyimbo za Injili katika Fasihi ya Kiswahili: Mifano Kutoka katika Nyimbo za Rose Muhando.
Masters thesis, The Open University Of Tanzania.
Abstract
Utafiti huu unahusu nafasi ya nyimbo za Injili katika fasihi ya Kiswahili: mifano kutoka katika nyimbo za Rose Muhando. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa nikuchunguza nafasi ya nyimbo za Injili katika fasihi ya Kiswahili kwa kutumia mifano ya nyimbo za Rose Muhando ili kuonesha jinsi msanii anavyotumia lugha kisanii katika nyimbo zake na kuibua dhamira za nyimbo hizo. Utafiti huu ulitumia
mbinu tatu za ukusanyaji wa data ambazo ni; usomaji wa machapisho, usaili na majadiliano ya vikundi. Aidha, sampuli ya utafiti huu iliteuliwa kwa kutumia mbinu
ya uteuzi wa madhumuni maalum. Uchambuzi wa data ulifanyika kwa kutumia mbinu ya uchambuzi maudhui. Utafiti huu pia umetumia nadharia ya simiotiki na kihemantiki katika kuchunguza, kuchambua na kujadili data za utafiti huu.Matokeo ya utafiti huu yamedhihirisha kuwa, msanii anatumia vipengele vya lugha kisanii katika kuwasilisha dhamira mbalimbali zinazosawiri uhalisia wa jamii. Aidha,
matokeo yanaonesha kuwa, nyimbo za Injili zina mchango mkubwa katika fasihi ya Kiswahili. Kazi yoyote ya fasihi huwa na dhima ya kufunza, kuadibisha, kuburudisha, kukosoa, kuelimisha na kuonya jamii. Hii ina maana kuwa, kazi ya
fasihi huibua uhalisia wa maisha ya jamii ambayo imemzaa, imemlea na kumkuza msanii wa kazi ya fasihi. Utafiti huu ulibaini kuwa, nyimbo za Injili kama kazi za fasihi huwasilisha uhalisia ulio ndani ya jamii, huelezea maisha ya jamii na kuyahusisha na maisha baada ya uhai. Kwa hiyo, data za utafiti huu zilidhihirisha kuwa nyimbo za Injiri si kwamba zinahusu dini tu bali ni nyimbo ambazo zina dhima
ya kifasihi katika jamii. Nyimbo hizi huelimisha, huonya, huadibu na pia huburudisha jamii. Hii ina maana kuwa, watu ndani ya jamii hutumia nyimbo za Injili
Actions (login required)
|
View Item |