Itikadi katika Tamthiliya za Emmanuel Mbogo: Utafiti Linganishi wa Ngoma ya Ng’wanamalundi na Fumo Liongo

Mhangilwa, Salome Clemence (2015) Itikadi katika Tamthiliya za Emmanuel Mbogo: Utafiti Linganishi wa Ngoma ya Ng’wanamalundi na Fumo Liongo. Masters thesis, The Open University Of Tanzania.

[thumbnail of DISSERTATION_-_SALOME_MHANGILWA_CLEMENCE_-_DISSERTATION.pdf]
Preview
PDF
Download (194kB) | Preview

Abstract

Kazi hii ilihusika na mada inayohusiana na Kuchunguza mbinu za kitanzia za Ki-Aristotle katika Tamthiliya za Fumo Liongo na Sundiata. Malengo mahususi ya utafiti huu yalikuwa ni kuchambua matumizi ya mbinu za tanzia za Kiaristotle katika tamthiliya ya Fumo Liongo na Sundiata, kuelezea matumizi ya mbinu ambazo si za tanzia za Ki-Aristotle katika tamthiliya teule na kuchambua dhamira katika tamthiliya za Fumo Liongo na Sundiata. Data za utafiti zimekusanywa kwa kutumia mbinu ya usomaji makini na kuchambuliwa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo na nadharia ya tanzia ya Ki-Aristotle. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa, mbinu za Ki-Aristotle zinazojitokeza katika tamthiliya teule ni msuko, wahusika, dhamira, fikra, utumiaji wa jukwaa na mtungo wa tamthiliya. Mbinu zisizo za Ki-Aristotle ni utendi, usimuliaji, diolojia, monolojia, majigambo na kuchanganya ushairi na nathari. Kwa upande wa dhamira zilizojitokeza katika tamthiliya teule ni uongozi kandamizi, rushwa katika jamii, usaliti, matabaka, nafasi ya mwanamke na ushirikina katika jamii.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 13 Jul 2016 10:28
Last Modified: 13 Jul 2016 10:28
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/1330

Actions (login required)

View Item View Item