Omchamba, Deusdedith I.
(2015)
Tathmini ya nafasi ya Lugha za Kijamii katika Fasihi ya Kiswahili: Mifano kutoka Riwaya ya Bwana Myombekere na Bibi Bugonoka Ntulinalwo na Bunalihwali.
Masters thesis, The Open University Of Tanzania.
Abstract
Utafiti huu unahusu Tathmini ya Nafasi ya Lugha za Kijamii katika Fasihi ya Kiswahili: Mifano kutoka Riwaya ya Bwana Myombekere na Bibi Bugonoka Ntulinalwo na Bunalihwali. Lengo lilikuwa ni kutathimini nafasi ya lugha za
Kiafrika katika fasihi ya Kiswahili ili kubaini jinsi vipengele vya utamaduni vilivyotumika katika kuibua dhamira ya kazi za fasihi ya Kiswahili. Katika kufikia
lengo hilo, utafiti huu ni wa maktabani ambao umetumia mbinu ya mapitio ya machapisho katika kukusanya data. Aidha, mbinu ya uchambuzi dhamira ilitumika katika kuchambua data za utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yanadhihirisha kuwa, mwandishi ametumia vipengele vya lugha kama vile; tamathali za semi, mdokezo, uchanganyaji wa lugha, misemo, methali na lugha ya picha. Utafiti huu umebaini kuwa, riwaya hii ni ya kiutamaduni ambayo inatumia lugha kisanii kuwasilisha dhamira ya jamii ya Wakerewe. Aidha, utafiti huu unaiona riwaya hii kama moja ya
riwaya za jamii za Kiafrika ambazo zinatumia lugha ya Kiswahili katika kusawiri maisha ya jamii za Kiafrika, mila, desturi, kaida na imani zake. Kwa kutumia utamaduni wa Kikerewe msanii ameweza kuibua dhamira ya uzazi na jinsi jamii inavyotazama mahusiano ya uzazi na kuzaa katika jamii. Aidha, msanii anatumia lugha kisanii kubainisha namna majina ya jamii hiyo yanavyotolewa kulingana na
maana zinazokubalika katika jamii. Kwa hiyo, utafiti huu umebaini kuwa, riwaya hii inadhihirisha nafasi ya lugha za Kiafrika katika fasihi ya Kiswahili ambapo inaonesha kuwa inafunza, kuonya, kuelimisha na kutunza amali za jamii hususani mila na desturi za jamii iliyoandikiwa raiwaya hiyo.
Actions (login required)
|
View Item |