Muhando, Roxana Eliamini
(2015)
Kuchunguza Dhamira za Kijamii katika Tamthiliya ya Kiswahili: Mfano wa Tamthiliya ya Hatia ya Penina Mlama.
Masters thesis, The Open University Of Tanzania.
Abstract
Mada ya utafiti huu ni kuchunguza dhamira za kijamii katika tamthiliya ya Kiswahili: Mfano wa Tamthiliya ya Hatia ya Penina Mlama. Katika harakati za kuishughulikia mada hii utafiti ulikuwa na malengo mahususi matatu ambayo ni kuelezea dhamira za kijamii zinazojitokeza katika tamthiliya ya Hatia iliyoandikwa na Penina Mlama, kutathimini uhalisia wa dhamira za kijamii zinazojitokeza katika tamthiliya ya Hatia kwa jamii ya leo ya Watanzania na kuchambua mbinu za kisanaa zilizotumika katika kuwasilisha dhamira za kijamii katika tamthiliya ya Hatia. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa katika tamthiliya ya Hatia kunajitokeza dhamira za kijamii kama vile, kusema uongo katika jamii, penye ukweli uongo hujitenga, nafasi ya mwanamke katika jamii, umasikini katika jamii na matabaka katika jamii. Dhamira zote hizo zimeonekana kuwa na uhalisia katika maisha ya kila siku ya jamii ya Watanzania. Pamoja na dhamira hizo pia katika tamthiliya ya Hatia tumebaini matumizi ya mbinu mbalimbali za kisanaa katika kuwasilisha dhamira mbalimbali. Mbinu hizo ni pamoja na matumizi ya nyimbo, takriri, tafsida na muundo wa moja kwa moja.
Actions (login required)
|
View Item |