Kuchunguza Usawiri Chanya wa Mwanamke Katika Vitendawili Vya Jamii ya Wanyiha

Kawia, Mshana Samwel (2015) Kuchunguza Usawiri Chanya wa Mwanamke Katika Vitendawili Vya Jamii ya Wanyiha. Masters thesis, The Open University Of Tanzania.

[thumbnail of DISSERTATION_-_MSHANA_SAMWEL_FINAL.pdf]
Preview
PDF
Download (729kB) | Preview

Abstract

Utafiti huu ulilenga kuchunguza usawiri chanya wa mwanamke na ujumbe unaopatika katika vitendawili vya jamii ya Wanyiha wanaoishi katika wilaya ya Mbozi mkoa wa Mbeya. Tasnifu hii imekusanya vitendawili kutoka katika Kata za Msia, Wasa, Igamba na Halungu, vijiji vinne vilihusishwa ambavyo ni; Igamba, Msia, Halambo na Wasa. Utafiti huu ulitumia nadharia tatu; kwanza, nadharia ya ndani-nnje ambayo ilitusaidia namna ya kuingia masikanini na kumakinika na wenyeji, kiasi cha kupunguza ugeni wa mtafiti. Nadharia hii, ilimsaidia mtafiti kupata uhusiano mzuri kati yake na watafitiwa. Pili, Nadharia ya ufeministi ilituongoza kuchunguza namna jamii ya Wanyiha inavyowasawiri wanawake katika mfumo mzima wa maisha. Tatu, Nadharia ya uhalisiya ilituongoza kuchunguza ujumbe unaopatikana katika vitendawili vya jamii ya Wanyiha. Nadharia ya ufeministi na uhalisia zilikuwa mwafaka katika hatua ya uwasilishaji na uchambuzi wa data. Mbinu tatu zilitumika katika hatua ya ukusanyaji wa data. Mbinu ya mahojiano, mbinu ya umakinifu na mbinu ya Udurusi wa nyaraka maktabani. Jumla ya vitendawaili arobaini vilikusanywa, vitendawili vitano viliteuriwa ili kutusaidia kutafuta majibu ya utafiti huu. Utafiti umepata majibu kwamba, vitendawili katika jamii hiyo humsawiri mwanamke katika hali mchanganyiko, chanya na hasi. Kwa hiyo, utafiti wetu umepata majibu kwamba, vipo vitendawili vyenye mtazamo chanya kuhusu mwanamke. Ujumbe unaopatikana katika vitendawili ni kwamba, mwanamke anapaswa kuthaminiwa sawa na mwanaume.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 13 Jul 2016 10:30
Last Modified: 13 Jul 2016 10:30
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/1317

Actions (login required)

View Item View Item