Etimolojia ya Majina ya Mahali ya Kaskazini Pemba Kuwa Utambulisho wa Utamaduni wa Wapemba

Zubeir, Zuwena Suleiman (2015) Etimolojia ya Majina ya Mahali ya Kaskazini Pemba Kuwa Utambulisho wa Utamaduni wa Wapemba. Masters thesis, The Open University Of Tanzania.

[thumbnail of DISSERTATION_-_BI_ZUWENA_FINAL.pdf]
Preview
PDF
Download (548kB) | Preview

Abstract

Utafiti huu ulihusu Etimolojia ya majina ya mahali. Ulichunguza etimolojia ya majina ya mahali ya Kaskazini Pemba kuwa utambulisho wa utamaduni wa Wapemba. Mtafiti aliongozwa na malengo matatu. Kwanza, kubainisha etimolojia ya majina ya mahali yanayopatikana Kaskazini Pemba; pili, kufafanua vigezo vinavyotumika kutoa majina ya mahali ya Kaskazini Pemba; na tatu, kubainisha utamaduni wa Wapemba jinsi ulivyoakisiwa na majina ya mahali ya Kaskazini Pemba. Ili kufikia lengo kuu lililokusudiwa mbinu mbali mbali za utafiti zilihusika. Mbinu hizo ni pamoja na mahojiano, hojaji pamoja na mjadala wa vikundi. Utafiti huu uliongozwa na nadharia jumuishi ambayo iliakisi data za utafiti huu kutokana na maoni yaliyotolewa na watafitiwa na wanajamii kwa ujumla yaliunda data za utafiti huu. Kwa upande wa matokeo ya utafiti, mtafiti aligundua kuwa majina ya mahali yana mfungamano na jamii na utamaduni wa jamii husika. Baadhi ya majina yanaakisi moja kwa moja shughuli wanazofanya wanajamii. Pia amebaini kuwa baadhi ya majina huwa ni ya hali ya kimazingira ya maeneo hayo kama jiografia inavyoonekana. Hata hivyo kuna majina ya mahali hutokana na watu maarufu au matendo ya kihistoria yaliyofanywa na wakazi wa zamani wa maeneo hayo. Mtafiti katika kazi yake amegundua pengo ambalo linahitaji kufanyiwa kazi, uibukaji wa majina mapya yanaathiri utamaduni wa jamii. Mtafiti anapendekeza kufanyika kwa utafiti utakaoeleza sababu zinazopelekea kuibuka kwa majina mapya ya mahali. Na pia maumbo ya majina ya mahali katika kipengele cha mofolojia na fonolojia kinaweza kufanyiwa utafiti kuona jinsi majina ya mahali yalivyo na maumbo mbali mbali.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 13 Jul 2016 10:35
Last Modified: 13 Jul 2016 10:35
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/1278

Actions (login required)

View Item View Item