Faki, Ali Mussa
(2015)
Kuchunguza Sifa za Kifani za Utendi wa Kiswahili: Mfano Utendi wa Fumo Liyongo.
Masters thesis, The Open University Of Tanzania.
Abstract
Utafiti huu unahusu kuchunguza sifa za kifani za Utendi au Utenzi wa Kiswahili. Utafiti huu ulichunguza vipengele vya fani kama vile; muundo, mtindo, wahusika, mandhari na matumizi ya lugha katika Utendi wa Kiswahili. Mfano, Utendi wa Fumo Liyongo, ili, kuona ni jinsi gani sifa za kifani zinavyojidhihirisha katika tenzi za Kiswahili. Utafiti huu ulitumia mbinu ya Maktaba. Wateuliwa wa utafiti huu walipatikana kwa kutumia mbinu ya madhumuni maalumu. Aidha, data za utafiti huu zilichambuliwa kwa kutumia mbinu ya kimaelezo. Utafiti huu umegundua kuwa tenzi za Kiswahili, zina sifa za kifani mahususi. Utafiti huu umegundua kuwa, neno na dhana tenzi ni sawa na tendi miongoni mwa jamii za Waswahili. Aidha, utafiti umegundua kuwa, tenzi za Kiswahili, zina sifa za kifani zinazofanana. Kwa mfano, zote zina mianzo na miishio inayofanana, ya kuanza kwa duwa na kumaliziya kwa duwa. Huwa na muundo na mtindo wa baharu ya Utendi. Utenzi, huweza kuwapo au kutakuwapo mhusika shujaa. Aidha, utafiti umegundua kuwa, tenzi za Kiswahili, hazia urefu mahususi au idadi maalumu ya beti. Sifa nyengine ni uunganifu na mapisi ya kweli. Pia, huwa una maudhui makubwa ya Dini ya Kiislamu. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Umuundo na Nadharia ya Ujumi wa Kiafrika katika kufikisha lengo lake.
Actions (login required)
|
View Item |