Saleh, Khatib Khamis
(2015)
Ufasihi Simulizi katika Riwaya za Shaaban Robert: Mifano kutoka Adili na Nduguze na Wasifu wa Siti Binti Saad.
Masters thesis, The Open University Of Tanzania.
Abstract
Utafiti huu unahusu ufasihi simulizi katika riwaya za Shaaban Robert kwa kutumia mifano ya riwaya: Mfano kutoka Adili na Nduguze na Wasifu wa Siti Binti Saad. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kufafanua vipengele vinavyojenga fasihi simulizi na jinsi vilivyotumika kuibua dhamira, na kutathmini na kubaini jinsi mtunzi huyo anavyofumbata mbinu ya mwingilianomatini katika kazi zake za fasihi, na namna mbinu hizo zinavyotumika kuibua dhamira za riwaya hizo.
Sampuli ya utafiti huu iliteuliwa kwa kutumia mbinu ya uteuzi wa madhumuni maalumu, nasibu na ile ya uteuzi rahisi, wakati ambapo data zilikusanywa kwa kutumia mbinu nne, ambazo ni mapitio ya maandiko, usaili, dodoso na majadiliano ya vikundi. Uchambuzi wa data ulifanyika kwa kutumia mbinu ya uchambuzi maudhui. Aidha nadharia ya mwingilianomatini ilitumika kukusanyia, kuchambua na kujadili data za utafiti huu.
Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa, mtunzi ametumia mbinu ya mwingilianomatini katika utunzi wake, pamoja na kuwa kazi hizo zina mpishano katika kutungwa kwake. Aidha, riwaya zote mbili ni matokeo ya athari za mapokeo ya matumizi ya fasihi simulizi ya Kiafrika, ambapo mtunzi ameathiriwa na masimulizi ya hadithi za fasihi simulizi na masimulizi ya kawaida katika utunzi wa riwaya ya Adili na Nduguze na Wasifu wa Siti Binti Saad.
Actions (login required)
|
View Item |