Kuchunguza dhima za vitendawili vya jamii ya Wanyisanzu wa Iramba, Singida, Tanzania

Damka, Amos Ben (2015) Kuchunguza dhima za vitendawili vya jamii ya Wanyisanzu wa Iramba, Singida, Tanzania. Masters thesis, The Open University Of Tanzania.

[thumbnail of Damka_thesis_submission.doc] PDF
Download (473kB)

Abstract

Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni Kuchunguza dhima za vitendawili vya jamii ya Wanyisanzu wa Iramba, Singida, kabla na baada ya uhuru wa Tanganyika, 1961. Aidha, utafiti ulitaka kujua dhima za vitendawili vya jamii ya Wanyisanzu, na kuchunguza vipengele vya fani vilivyosababishwa na mabadiliko ya kutega vitendawili katika jamii ya Wanyisanzu. Utalii wa kazi tangulizi uliongozwa na nadharia ya kuchunguza dhima za vitendawili katika jamii ya Wanyisanzu. Utafiti umetumia mbinu ya ushiriki, mahojiano, maswali ya hojaji na utalii wa nyaraka zilizotumika kukusanyia data za utafiti.Aidha, mbinu ya uchambuzi wa kimaelezo ndiyo iliyotumika katika uchambuzi wa data. Eneo la utafiti lilikuwa ni Nkata ya Nkinto na Mwangeza, wilaya ya Iramba, mkoa wa Singida. Matokeo ya utafiti yamebainisha kushuka kwa dhima za vitendawili katika jamii ya Wanyisanzu.Chanzo cha kushuka kwa dhima ya vitendawili ni; Mabadiliko ya kisomo shuleni, yamesababisha matumizi makubwa zaidi ya lugha ya Kiswahili na kusahaulika kwa lugha za asili zilizotumika, kutegea na kutegulia vitendawili. Pili, Mabadiliko ya shughuli za kiuchumi kama vile, biashara na kilimo, zimesababisha watu kutokukusanyika pamoja saa za jioni. Mwisho, kuibuka kwa ugeni wa tekinolojia (utunduizi), kumeleta mabadiliko, siyo ya kuhifadhi vitendawili kwenye maandishi, Mitandao-CD na flashi.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 13 Jul 2016 10:49
Last Modified: 13 Jul 2016 10:49
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/1201

Actions (login required)

View Item View Item