Makame , Mussa Khamis
(2015)
Uchambuzi wa Viangama Katika Kiswahili cha Mazungumzo Unguja.
Masters thesis, The Open University Of Tanzania.
Abstract
Utafiti huu unaohusu uchambuzi wa viangama katika Kiswahili cha mazungumzo lengo lake kuu ni kuchambua viangama katika Kiswahili cha mazungumzo Unguja. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya viangama ya Zwicky (1977) amechambua viangama sahili, viangama maalumu na viangama funge. Utafiti umetumia mbinu mbalimbali katika ukusanyaji wa data zake. Utafiti umefanyika Unguja mjini katika shehia nne ambazo ni Shangani, Mchangani, Mwanakwerekwe na Mombasa. Walengwa wa utafiti huu ni wazee, watu wa makamo na vijana. Kila shehia wamesailiwa watu 25 wa umri na jinsia tafauti na kufanyiwa usaili watu 100.. Utafiti huu umetumia mbinu za hojaji, usaili na ushuhudiaji. Utafiti umetumia data simulizi ambapo mtafiti amefanya usaili na kushuhudia kwa kusikiliza mazungumzo kutoka mikusanyiko ya watu mbalimbali. Kwa upande wa uchambuzi wa data, mtafiti amechambua aina za viangama tamati zilizomo katika Kiswahili cha mazungumzo, maumbo ya viangama tamati katika Kiswahili cha mazungumzo na kategoria za maneno ambazo ni viegemewa vya viangama tamati katika Kiswahili cha mazungumzo. Kwa upande wa matokeo ya utafiti, data zimeonesha kuwa Kiswahili cha mazungumzo kina viangama tamati vyenye maumbo yafuatayo: viwakilishi, vimilikishi, viulizi, vivumishi, viunganishi na vielezi. Maumbo hayo yameegemezwa kwenye nomino, vitenzi, vielezi na viwakilishi. Kwa upande wa mapendekezo mtafiti amependekeza ufanyike utafiti wa Kiswahili cha mazungumzo Unguja na lahaja ya Kipemba. Pia anapendekeza ufanyike utafiti wa viangama awali katika Kiswahili cha mazungumzo. Vile vile amependekeza ufanye utafiti linganishi baina ya Kiswahili cha mazungumzo na lugha za Kibantu. Mwisho amependekeza ufanywe utafiti wa viangama awali vya Kiswahili sanifu.
Actions (login required)
|
View Item |