Tofauti za Msamaiti Baina ya Kiswahili cha Chake Chake na Kiswahili cha Micheweni katika Kisiwa cha Pemba

Ali, Shaame Ismail (2015) Tofauti za Msamaiti Baina ya Kiswahili cha Chake Chake na Kiswahili cha Micheweni katika Kisiwa cha Pemba. Masters thesis, The Open University Of Tanzania.

[thumbnail of ismail_alli__-__Dissertation___-__Final_(3).doc] PDF - Submitted Version
Download (728kB)

Abstract

Lengo la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza tofauti za msamiati baina ya Kiswahili kizungumzwacho Micheweni na Chake Chake katika kisiwa cha Pemba. Utafiti ulitumia data za uwandani; watoa data walikuwa; watu wazima, wanawake na wanaume wenye umri kuanzia miaka 45. Data zimekusanywa kwa kutumia mbinu ya usaili na hojaji na sampuli tegemea fursa imetumika kuchagua watoa taarifa kwa vigezo vya umri na ukaazi. Nadharia ya isimu linganishi na mbinu ya uchambuzi linganishi zimetumika kuchambua data za utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kuwa kuna tofauti kubwa ya msamiati baina Kiswahili cha Chake Chake na Micheweni katika kisiwa cha Pemba.Tofauti zilizobainika zaidi zinahusu matamshi na maumbo ya maneno na chache zinahusu maana. Pia imebainika kuwa kuna baadhi ya matumizi ya msamiati unaolingana baina ya maeneo hayo. Aidha, utafiti huu umegundua kuwa licha ya tofauti kubwa iliyopo ya msamiati wa Ki-Micheweni na Ki-Chake Chake katika matamshi na maumbo ya maneno kuna kufanana kwa kiwango kikubwa kimaana. Kutokana na matokeo ya utafiti huu mapendekezo yafuatayo yametolewa; Wanataaluma wenye nia ya kuandika kuhusu isimu ya Kiswahili kizungumzwacho katika kisiwa cha Pemba, hasa wenye dhamira ya kuchambua misamiati ya Kiswahili cha Chake Chake, cha Michweni, na maeneo mengine yanayofanana watumie matokeo ya utafiti huu kama muongozo wa kuandika isimu sahihi ya Kiswahili. Pia walimu na wanafunzi watumie matokeo ya utafiti huu kama marejeo ya kupata msamiati wa Kiswahili cha Micheweni na Chake Chake katika kisiwa cha Pemba. Vile vile taasisi zinazohusika na kuhifadhi maneno ya Kiswahili watamie matokeo ya utafiti huu kuhifadhi msamiati wa Kiswahili cha Micheweni na yale ya Kiswahili cha Chake Chake katika maandishi.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 13 Jul 2016 10:52
Last Modified: 17 Oct 2018 13:15
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/1177

Actions (login required)

View Item View Item