Ushujaa wa Shujaa wa Motifu za Safari na Msako Katika Ngano za Waikizu, Wabondei na Wazanzibari

Nyamsenda, Jane Chacha (2015) Ushujaa wa Shujaa wa Motifu za Safari na Msako Katika Ngano za Waikizu, Wabondei na Wazanzibari. ["eprint_fieldopt_thesis_type_phd" not defined] thesis, The Open University Of Tanzania.

[thumbnail of JANE_PHD_EXTERNAL_EXAMINER_final.doc] PDF
Download (4MB)

Abstract

Lengo kuu la utafiti huu, lilikuwa ni kubainisha nduni bainifu za Ushujaa wa Shujaa wa Motifu za Safari na Msako katika ngano za Waikizu. Utafiti huu umefanywa Ikizu. Njia zilizotumika katika utafiti huu zilikuwa ni utafiti wa Maktabani na uwandani. Nadharia zilizotumika katika utafiti huu ni; Umuundo, Saikochanganuzi, Sosholojia na nadharia ya Vikale. Matokeo ya Utafiti huu yamebaini mambo yafuatayo: Kwanza, Ushujaa wa masafa marefu. Ambapo shujaa hupambana na hali na mazingira halisi ana kwa ana. Pili, Safari ya shujaa ambapo shujaa huondoka peke yake nyumbani na hurudi peke yake nyumbani. Na kama shujaa atarudi nyumbani na watu, huwa ni wale aliokwenda kuwapigania. Tatu, shujaa ni lazima arudi nyumbani, kama shujaa hatarajii kurudi nyumbani basi huyo siyo shujaa. Nne, ngano za motifu za safari na msako hutumika kuelezea na kusisitiza utamaduni, falsafa, mazingira, imani, jiografia, historia na maisha ya Waikizu. Tano, nimegundua tofauti za kitamaduni, kijamii, kihistoria, kijiografia, kimazingira kifalsafa na tofauti za kaida mbalimbali za kijamii. Nimebaini kwamba tofauti hizi, ndizo sababu ya tofauti za ushujaa wa Waikizu, Wabondei na Wazanzibari. Sita, motifu ya safari na motifu ya msako zinauhusiano, maana zinajengana, zinaathiriana na kukamilishana, kama ilivyo sarafu moja yenye pande mbili tofauti. Saba, kuna uhusiano wa moja kwa moja baina ya mashujaa wa tendi na mashujaa wa ngano. Nane, katika utafiti huu imebainika kuwa, katika ngano za Waikizu kuna mashujaa wa kike na mashujaa wa kiume. Tisa, Utafiti huu umebaini nguvu ya mwanamke katika kuathiri nguvu za shujaa. Hivyo mapendekezo yangu kwa watunga sera ni kwamba, wachukue hatua za kuimarisha utafiti na mafunzo katika nyanja ya fasihi simulizi ya Kiafrika ili kupanuawigo wa maarifa katika ngazi zote za elimu.

Item Type: Thesis (["eprint_fieldopt_thesis_type_phd" not defined])
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 13 Jul 2016 10:53
Last Modified: 13 Jul 2016 10:53
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/1175

Actions (login required)

View Item View Item