Msacky, Eva Yeronimo
(2015)
Kuchunguza Dhamira za Kijamii na Kisiasa katika Riwaya ya Siri za Maisha.
Masters thesis, The Open University Of Tanzania.
Abstract
Mada ya utafiti huu ni kuchunguza dhamira za kijamii na kisiasa katika riwaya ya Siri za Maisha. Malengo mahususi ya utafiti huu yalikuwa ni kuchambua dhamira za kijamii zinazojitokeza katika riwaya ya Siri za Maisha, kuchambua dhamira za kisiasa zinazojitokeza katika riwaya ya Siri za Maisha na kuelezea mbinu za kisanaa zinazowasilisha dhamira za kijamii na kisiasa katika riwaya ya Siri za Maisha. Ili kukamilisha malengo haya mahususi, data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia mbinu za usomaji makini na upitiaji wa nyaraka na kuchambuliwa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo na nadharia za Simiotiki na Saikolojia Changanuzi.
Utafiti umepata matokeo yanayoonesha kuwa katika riwaya ya Siri za Maisha kuna dhamira za kijamii kama vile umasikini, ulevi na uvivu na uzembe. Dhamira za kisiasa ni ukombozi wa kifikra, usawa wa binadamu na nafasi ya mwanamke katika jamii. Mbinu za kisanaa zilizotumiwa na mwandishi kuwasilishia dhamira hizi ni mbinu za kidrama, kishairi, sitiari na misemo.
Actions (login required)
|
View Item |