Matatizo Wanayoyapata Wanafunzi Walibya katika Kujifunza Viambishi vya Njeo katika Lugha ya Kiswahili

Mohammed, Jabir Alzarok Jabir (2010) Matatizo Wanayoyapata Wanafunzi Walibya katika Kujifunza Viambishi vya Njeo katika Lugha ya Kiswahili. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of JABIR_ALZAROK_JABIR_MOHAMMED.pdf]
Preview
PDF
Download (1MB) | Preview

Abstract

Utafiti huu wa 'Matatizo Wanayopata Wanafunzi Walibya katika Kujifunza Viambishi vya Njeo katika Kiswahili' ni wa kwanza na wa aina yake katika ulimwengu wa lugha ya Kiswahili. Hii ni kwa sababu kwa mara ya kwanza sasa tunapata utafiti unaohusu baadhi ya matumizi yanayowakwamisha wanafunzi wengi kama vile Walibya kujifunza kurnudu lugha ya Kiswahili ipasavyo. Kama jina la utafiti linavyoashiria, utafiti huu umefanywa ili kuonyesha mojawapo ya matatizo yanayowakabili Wanafunzi Walibya wanaojifunza Kiswahili na kwa kiasi fulani walimu wanaowafundisha lugha hiyo. Nia hasa, ni kuonyesha undani wa tatizo hili na jinsi linavyoweza kutatuliwa ili kuwasaidia hasa wanafunzi kumudu vizuri masuala ya kisarufi ya Kiswahili Sanifu wakati wanajifunza. Ni dhahiri kwamba matokeo ya utafiti huu pia yatawasaidia walimu wanaowafundisha wanafunzi wenye asili ya Libya kuelewa misingi ya kisarufi ya lugha hii kwa haraka na kwa ufanisi. Maelezo haya yatafanywa katika sura tano kwa utaratibu ufuatao: Sura ya Kwanza itakuwa ni utangulizi unaoonyesha tatizo la utafiti, malengo ya utafiti, na mbinu zilizotumika katika utafiti. Sura hii pia inapitia maandishi mbalimbali hasa yale yaliyohusu viambishi vya njeo na kuweka nadharia tete za utafiti. Sura hii pia itatazama masuala ya kinadharia yanayohusiana na ufundishaji wa lugha ya pili. Sura ya Pili inachunguza kwa undani maumbile muhimu ya sarufi ya Kiswahili, hususani maumbo yanayojitokeza kuhusiana na viambishi vya njeo na maana zinazojitokeza zinazofanya matumizi yenye viambishi hivi kuwatatiza wanafunzi. Sura ya Tatu itatalii maumbile ya lugha ya Kiarabu na kubainisha athari zinazoweza kutokea kutokana na maumbo na mipangilio ya kisarufi katika lugha hii. Maelezo katika sura hii yatawasaidia walimu na wanafunzi kulinganisha masuala ya kisarufi baina ya lugha hizi wanazokabiliana nazo. Sura ya Nne itachanganua msingi ya matatizo ya viambishi vya njeo kwa wanafunzi wa Libya wanaojifunza Kiswahili. Sura ya tano itatoa hitimisho na mapendekezo mbalimbali.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 900 History, geography, (& biography)
Divisions: Faculty of Law > Faculty of Law
Depositing User: Mr. Administrator OUT
Date Deposited: 14 Sep 2011 12:14
Last Modified: 18 Jun 2013 09:35
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/164

Actions (login required)

View Item View Item