Kuchunguza Masuala ya Kisiasa Katika Riwaya za Shaaban Robert: Mfano wa Kusadikika na Kufikirika

Massawe , Bibiana (2014) Kuchunguza Masuala ya Kisiasa Katika Riwaya za Shaaban Robert: Mfano wa Kusadikika na Kufikirika. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of BIBIANA_MASSAWE_AMBROSE.pdf]
Preview
PDF
Download (399kB) | Preview

Abstract

Mada ya utafiti huu ilikuwa ni kuchunguza masuala ya Kisiasa katika Riwaya za Shaaban Robert: Mfano wa Kusadikika na Kufikirika. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kutathimini masuala ya kisiasa katika riwaya za Shaaban Robert kupitia riwaya za Kusadikika na Kufikirika. Lengo kuu la utafiti huu limefikiwa baada ya madhumuni mahususi matatu kukamilika. Madhumuni hayo ni Kubainisha masuala ya kisiasa katika riwaya za Shaaban Robert, Kubainisha mchango wa Shaaban Robert katika maendeleo ya kisiasa nchini Tanzania na kuchunguza mbinu za kisanaa zinazotumiwa na Shaaban Robert kusawiri masuala ya kisiasa katika Kusadikika na Kufikirika. Data za utafiti huu zilikusanywa kwa kutumia mbinu za usaili na uchambuzi wa kimaudhui. Mikabala wa kidhamira na kimaelezo ndio iliyotumika kuchambua data za utafiti huu. Utafiti umebaini kuwa, masuala ya kisiasa yanayojitokeza katika riwaya za Kusadikika na Kufikirika ni uongozi mzuri, uongozi mbaya, utii wa sheria, masuala ya jinsia na kujifunza kutoka kwa wengine. Masuala haya yanawasilishwa na Shaaban Robert kwa kutumia mbinu za kisanaa za matumizi ya methali, misemo,tashibiha, kejeli, mandhari ya kidhanaishi na wahusika bapa. Masuala ya kisiasa yanayowasilishwa na Shaaban Robert yametoa mchango mkubwa katika kuimarisha uongozi wa nchi huru ya Tanganyika na baadae Tanzania.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 410 Linguistics
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr. Administrator OUT
Date Deposited: 12 Nov 2015 06:44
Last Modified: 24 May 2017 14:05
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/444

Actions (login required)

View Item View Item