Kuchunguza Maendeleo ya Ubunifu katika Tamthilia ya Kiswahili

Masatu, Furaha (2023) Kuchunguza Maendeleo ya Ubunifu katika Tamthilia ya Kiswahili. Doctoral thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of FURAHA J. MASATU EDITED PHD THESIS FINAL REPORT 2023 - Copy.pdf] PDF - Submitted Version
Download (1MB)

Abstract

Utafiti huu ulijikita katika kuchunguza maendeleo ya ubunifu katika Tamthilia ya Kiswahili kwa kulinganisha tamthilia za awamu ya Azimio la Arusha na soko huria nchini Tanzania. Lengo lilikuwa ni kulinganisha kazi za awamu mbili tofauti ili kubaini kufanana na kutofautiana katika ubunifu wa ujenzi wa dhamira na matumizi ya lugha ili kubaini kama kuna maendeleo endelevu ama la. Utafiti ulimakinikia dhamira, matumizi ya ucheshi, matumizi ya misimu, matumizi ya uchanganyaji ndimi na uwepesi na ugumu wa lugha. Kiunzi cha utafiti kilikuwa ni nadharia ya Fasihi Linganishi. Utafiti ulikuwa ni wa maktabani. Tamthilia sita za Kiswahili (Mashetani, Kijiji Chetu, Harakati za Ukombozi, Safari ya Chinga, Changamoto na Nje – Ndani) ziliteuliwa kwa kutumia mbinu ya usampulishaji nasibu tabakishi. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya usomaji makini. Uchambuzi wa data na uwasilishaji wa matokeo ya utafiti uliongozwa na mkabala wa kiufafanuzi. Matokeo ya utafiti yanadhihirisha kuwa, waandishi wa tamthilia teule wanafanana na kutofautiana katika uteuzi na ujenzi wa dhamira na lugha ya tamthilia zao. Ubunifu katika kila tamthilia teule umethibitika kwenda na wakati, hali, lengo la utunzi na mazingira ya utunzi. Kila mwandishi ameonesha upya wa kipekee katika kazi yake. Hivyo, utafiti huu umebaini kuwa siyo kweli kwamba tamthilia za Kiswahili za nchini Tanzania ambazo watunzi wake ni zao la awamu ya soko huria hazina ubunifu endelevu. Kwa hiyo basi, tafiti zaidi zinahitajika kuhusu tamthilia za Kiswahili ambazo watunzi wake ni zao la awamu ya soko huria ili kuondoa ombwe la taarifa za msingi katika kutathmini historia na maendeleo ya Tamthilia ya Kiswahili nchini Tanzania. Maneno muhimu ni dhamira, maendeleo, misimu, ubunifu, uchanganyaji ndimi, ucheshi, uwepesi na ugumu wa lugha.

Item Type: Thesis (Doctoral)
Subjects: 400 Language > 410 Linguistics
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Khadija Katele
Date Deposited: 31 Jul 2024 10:22
Last Modified: 31 Jul 2024 10:22
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/3890

Actions (login required)

View Item View Item