Aghel, Abdalla M.
(2021)
Ulinganishi wa Mofolojia ya Vitenzi vya Kiswahili na Kiarabu.
Doctoral thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Utafiti huu ulijikita katika ulinganishi wa mofolojia ya vitenzi vya mofolojia ya vitenzi vya Kiswahili na Kiarabu kwa kuzingatia vipengele vya wakati, nafsi, ukanushi na kauli. Utafiti huu ulitumia mkabala wa Kihistahilifu linganishi kwa kuwa ulihusu ulinganishi wa mofolojia ya vitenzi vya Kiarabu na Kiswahili. Pia ulitumia nadharia ya Umbo Upeo ambayo imejengwa katika misingi mitatu, wa kwanza unaitwa zalishi (ZALI), wa pili unajulikana kama masharti zuizi (MASHA- ZU) na wa tatu ni tathmini (TATHI). Data zilizotumika katika utafiti huu zilitokana na vyanzo vya maktaba pamoja na za uwandani ambazo zilipatikana kwa mbinu ya mahojiano baina ya mtafiti na wazungumzaji wa lugha za Kiswahili na Kiarabu katika Chuo Kikuu cha Tripoli, Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (CKTZ) pamoja na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT). Utafiti huu umebaini kwamba vitenzi vya lugha ya Kiswahili na Kiarabu vinatofautiana katika maumbo yake kutokana na namna vinavyoathiriwa na nafsi, ukanushi, kauli na wakati. Mfano, katika vitenzi vya silabi moja, mzizi wa kitenzi cha Kiswahili hunyumbuka katika maumbo mawili, yaani mzizi na mofimu tamati wakati kitenzi hicho katika lugha ya Kiarabu hakiwezi kunyumbuka katika maumbo mawili bali husimama kama mzizi peke yake. Vilevile, utafiti huu ulibaini kuwa mofimu ya nafsi ya kitenzi kutokea mwisho wa neno baada ya mzizi kutokana na kuathiriwa na kipengele cha nafsi tofauti na ilivyo katika lugha ya Kiswahili ambapo mofimu ya nafsi hutokea kabla ya mzizi wa neno. Hivyo, utafiti huu unahitimisha kuwa Kiarabu na Kiswahili ni lugha mbili tofauti zenye kanuni na maumbo tofauti kulingana na utamaduni na mazingira ya lugha hizi.
Maneno makuu: Mofolojia, umbo upeo, mzizi, mofimu
Actions (login required)
|
View Item |