Kuchunguza Usanaa wa Lugha katika Kujenga Dhima za Nyimbo za Harusi Katika Jamii ya Waasu

Yonazi, Elihaki (2019) Kuchunguza Usanaa wa Lugha katika Kujenga Dhima za Nyimbo za Harusi Katika Jamii ya Waasu. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASNIFU - ELIHAKI YONAZI - FINAL.pdf] PDF
Download (815kB)

Abstract

Utafiti huu unahusu kuchunguza usanaa wa lugha katika kujenga dhima za nyimbo za harusi katika jamii ya Waasu. Ili kutimiza lengo hilo tulikuwa na malengo mahsusi mawili; kuchunguza dhima za nyimbo za harusi katika jamii ya Waasu; na kujadili usanaa wa lugha unaotumika katika ujenzi wa dhima za nyimbo za harusi katika jamii ya Waasu. Data za utafiti zilikusanywa kwa mbinu za hojaji, ushiriki, usaili na ile ya kinyaraka. Mjadala wa data ulioongozwa na nadharia za Uhalisia na Simiotiki. Nadharia hizo zilikuwa muafaka katika uchambuzi na mjadala wa vipengele vilivyolengwa katika utafiti huu. Kipekee, nadharia hizi ziliteuliwa kwa misingi ya kutegemeana na kukamilishana ili kukidhi malengo mahsusi ya utafiti. Aidha, matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa nyimbo za harusi katika jamii ya Waasu zina dhima nyingi. Baadhi yake ni kudumisha upendo, kudumisha heshima, kupongeza na kuwasifu maharusi, kuhimiza ukarimu na ushirikiano, kurekebisha tabia, kuonesha masikitiko na uvumilivu na kuonya. Kimsingi, nyimbo hizo hutazamwa kama kiungo thabiti cha kijadi kinachohakiki na kujenga misingi ya kuifunza jamii na kuielewa historia, mila na desturi, pamoja na mazingira yao kwa kuzingatia maendeleo ya kijamii. Vipengele vya kisanaa vilivyochunguzwa ni; taswira na ishara, jazanda/mafumbo, chuku, tashibiha na takriri. Vipengele vingine ni dhihaka na methali. Usanaa wa katika vipengele hivyo umeonesha mchango mkubwa, unaoongeza nguvu na kujenga mvuto wa kipekee unaolenga kuihamasisha jamii kupata undani wa jambo lililolengwa.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 800 Literature > 800 Literature, rhetoric & criticism
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr. Administrator OUT
Date Deposited: 23 Sep 2021 09:26
Last Modified: 23 Sep 2021 09:26
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/3013

Actions (login required)

View Item View Item