Yonazi, Elihaki
(2019)
Kuchunguza Usanaa wa Lugha katika Kujenga Dhima za Nyimbo za Harusi
Katika Jamii ya Waasu.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Utafiti huu unahusu kuchunguza usanaa wa lugha katika kujenga dhima za nyimbo
za harusi katika jamii ya Waasu. Ili kutimiza lengo hilo tulikuwa na malengo
mahsusi mawili; kuchunguza dhima za nyimbo za harusi katika jamii ya Waasu; na
kujadili usanaa wa lugha unaotumika katika ujenzi wa dhima za nyimbo za harusi
katika jamii ya Waasu. Data za utafiti zilikusanywa kwa mbinu za hojaji, ushiriki,
usaili na ile ya kinyaraka. Mjadala wa data ulioongozwa na nadharia za Uhalisia na
Simiotiki. Nadharia hizo zilikuwa muafaka katika uchambuzi na mjadala wa
vipengele vilivyolengwa katika utafiti huu. Kipekee, nadharia hizi ziliteuliwa kwa
misingi ya kutegemeana na kukamilishana ili kukidhi malengo mahsusi ya utafiti.
Aidha, matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa nyimbo za harusi katika jamii ya Waasu
zina dhima nyingi. Baadhi yake ni kudumisha upendo, kudumisha heshima,
kupongeza na kuwasifu maharusi, kuhimiza ukarimu na ushirikiano, kurekebisha
tabia, kuonesha masikitiko na uvumilivu na kuonya. Kimsingi, nyimbo hizo
hutazamwa kama kiungo thabiti cha kijadi kinachohakiki na kujenga misingi ya
kuifunza jamii na kuielewa historia, mila na desturi, pamoja na mazingira yao kwa
kuzingatia maendeleo ya kijamii. Vipengele vya kisanaa vilivyochunguzwa ni;
taswira na ishara, jazanda/mafumbo, chuku, tashibiha na takriri. Vipengele vingine ni
dhihaka na methali. Usanaa wa katika vipengele hivyo umeonesha mchango
mkubwa, unaoongeza nguvu na kujenga mvuto wa kipekee unaolenga kuihamasisha
jamii kupata undani wa jambo lililolengwa.
Actions (login required)
|
View Item |