Migodela, Willy
(2020)
Kuchunguza Mtindo katika Nyimbo
za Tiba Asili: Mifano Kutoka Nyimbo za Waganga wa Mkoa wa Ruvuma.
["eprint_fieldopt_thesis_type_phd" not defined] thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Utafiti huu ulihusu ‘Kuchunguza Mtindo katika Nyimbo za Tiba Asili: Mifano
Kutoka Nyimbo za Waganga wa Mkoa wa Ruvuma’. Utafiti ulikuwa na malengo
mahsusi matatu. Lengo mahsusi la kwanza lilihusu kuainisha nyimbo za tiba asili za
waganga wa mkoa wa Ruvuma. Lengo mahsusi la pili lilihusu kubainisha mtindo wa
nyimbo za tiba asili za waganga wa mkoa wa Ruvuma. Lengo la tatu lilikuwa ni
kutathmini matokeo ya mtindo wa nyimbo za tiba asili kwa wagonjwa. Utafiti huu
uliongozwa na nadharia mbili za Mitindo na Simiotiki, pamoja na mbinu ya maelezo
ya kinathari. Matokeo yanaonesha kwamba, kuna aina saba za nyimbo za tiba asili
zinazotokana na dhima ya nyimbo hizo. Aina hizo ni nyimbo za maombi,
kuomboleza, kufurahisha mizimu, kueleza historia, shkurani, kutolea tiba na nyimbo
za kuaga. Vilevile, kuna mitindo mbalimbali inayotokana na matumizi na
viziaadalugha. Mitindo hiyo, inahusiana na matumizi ya lugha ya kawaida na lugha
ya kisanaa namatumizi ya nyimbo ndefu na fupi. Pia, kuna mishororo, fomula,
dailojia, vina na mizani, uchezaji, utendaji wa kimuziki na matumizi ya maleba na
vifaa. aidha, upo uhusiano wa moja kwa moja baina ya nyimbo na matibabu katika
tiba asili. Matokeo ya nyimbo hizo kwa wagonjwa yamebainika kuwa ni pamoja na
kuwatia moyo wagonjwa, kuwashirikisha katika mchakato wa tiba, kuburudika,
kuwaongezea imani ya tiba na kufukuza majini wabaya. Utafiti huu ni kwamba,
serikali ibuni sera za kuwaendeleza waganga wa tiba asili na kutoa kipaumbele
kwenye tafiti za kitamaduni ili kulinda amali za taifa. Watafiti wengine wanaweza
kufanya tafiti zaidi kuhusu maudhui ya nyimbo za
Actions (login required)
|
View Item |