Uwiano na Utofauti wa Kiisimu Kati ya Kiswahili cha Paje na Makunduchi

Abdallah, Shomari Said (2018) Uwiano na Utofauti wa Kiisimu Kati ya Kiswahili cha Paje na Makunduchi. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASINIFU YA SHOMARI  SAID ABDALLAH.pdf] PDF
Download (2MB)

Abstract

Utafiti huu uliangazia uwiano na utofauti wa kiisimu kati ya Kiswahili cha Paje na Makunduchi. Na ulikuwa na malengo matatu; Kubainisha mfanano na utofauti baina ya fonimu za Kiswahili cha Paje na Makunduchi, pili Kulinganisha na kutofautisha kanuni za kifonolojia na mofolojia zinazotawala mofu ziundazo maneno ya Kiswahili cha Paje na Makunduchi na Kubainisha uwiano na utofautiano wa kimaana baina ya msamiati wa Kiswahili cha Paje na Makunduchi. Ili kufikia malengo yaliyokusudiwa mbinu za usaili, hojaji, ushuhudiaji na Maktabani zilitumika, hata hivyo utafiti huu uliongozwa na nadharia mbili; isimu linganishi na Mofofonolojia pamoja na sampuli ya watoa taarifa sitini (60) ilitumika thelathini kutoka Paje na thelathini kwa Makunduchi. Kupitia matokeo ya utafiti, imegundulika kuwa Kifonolojia jamii hizi zinatofautiana kifonimi hasa kiidadi na kimatumizi kwa baadhi ya fonimu hizo. Pia, imebainika kuwa Kimakunduchi na Kipaje vinatofautiana katika baadhi ya kanuni za fonolojia na mofolojia kama vile katika udondoshaji na uyeyushaji katika baadhi ya nomino, vitenzi na vivumishi vimilikishi. Pia imebaainika kuwa Kimakunduchi na Kipaje vinatofautiana katika umiliki wa alomofu za nafsi ya kwanza na ya pili pamoja na viambishi vya ung'oekaji wa o-rejeshi, pamoja na hayo imebainika kuwa jamii hizi zinatofautiana kimaana katika baadhi ya maneno na hivyo imeonekana kuwa Wapaje wameathiriwa na Kiswahili sanifu katika utoaji na uwakilishi wa maana zao. Mwisho mtafiti amependekeza mambo kadhaa kwa watafiti wajao, mambo hayo ni pamoja na tafiti nyingine linganishi zifanyike kwa baadhi ya vipengele vya fonolojia vipande kama vile silabi, fonolojia arudhi pamoja na kipengele cha sintaksia. Pili tumebaini kuwa Kimakunduchi kina vilahaja zaidi ya kimoja hivyo mtafiti anapendekeza eneo hili ni vizuri likafanyiwa uchunguzi wa kiutafiti zaidi.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: UNSPECIFIED
Depositing User: Mr. Administrator OUT
Date Deposited: 21 Sep 2021 11:41
Last Modified: 21 Sep 2021 11:41
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2915

Actions (login required)

View Item View Item