Kuchunguza Dhamira katika Riwaya ya Kiswahili: Mifano kutoka katika Siku ya Watenzi Wote

Ali, Ali Omar (2018) Kuchunguza Dhamira katika Riwaya ya Kiswahili: Mifano kutoka katika Siku ya Watenzi Wote. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASINIFU YA ALI OMAR ALI.pdf] PDF
Download (412kB)

Abstract

Mada ya utafiti ni kuchunguza dhamira katika riwaya ya Kiswahili kwa kurejelea riwaya ya Siku ya Watenzi Wote ya mtunzi Shaaban Robert. Malengo mahususi ya utafiti yalikuwa mawili ambayo ni kuchambua dhamira katika riwaya ya Siku ya Watenzi Wote na kuelezea uhalisia wa dhamira za siku ya Watenzi Wote kwa jamii ya leo. Data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia mbinu za usomaji makini na upitiaji wa nyaraka na kuchambuliwa kwa kutumika mkabala wa kimaelezo na nadharia ya Saikolojia Changanuzi. Matokeo ya utafiti yanabainisha kuwa riwaya teule ina dhamira nyingi na sisi tumebainisha dhamira 7 ikiwa ni wasiwasi, ukoloni, malezi, kutimiza wajibu, umuhimu wa elimu na uzalishaji mali. Dhamira hizi zote zinaonekana kuwa zina lengo moja kuu la kumfanya binadamu kujitambua na kuweza kutekeleza majukumu yake ili kujiletea maendeleo katika jamii. Kisaikolojia dhamira hizi ni hai na kwamba licha ya riwaya husika kuandikwa takribani miaka 50 iliyopita lakini bado dhamira zake ni muafaka kwa kizazi cha leo na hata vizazi vijavyo. Uandishi wa aina hii ni wa hali ya juu sana ambao tunauona kwa mwandishi huyu pekee ukimlinganisha na waandishi wengine wa riwaya na fasihi ya Kiswahili kwa jumla. Mwishoni mwa tasinifu hii kumtolewa mapendekezo kwa ajili ya utafiti wa baadaye.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 800 Literature > 800 Literature, rhetoric & criticism
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr. Administrator OUT
Date Deposited: 21 Sep 2021 10:56
Last Modified: 21 Sep 2021 10:56
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2908

Actions (login required)

View Item View Item