Ali, Mwalimu Bakari
(2019)
Ulinganifu wa Midhihiriko na Matumizi ya Kiambishi “ka” na “ku” katika lahaja ya Kipemba.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Utafiti huu ulihusu Ulinganifu wa Midhihiriko na Matumizi ya Kiambishi “ka” na “ku” katika lahaja ya Kipemba. Lengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza ulinganifu wa midhihiriko na matumizi ya Kiambishi “ka” na “ku” katika lahaja ya Kipemba. Ili kufikia malengo, mbinu mbalimbali za utafiti zilihusika, mbinu hizo dodoso, hojaji na uchunguzi. Kwa upande wa matokeo ya utafiti; utafiti ulieleza kwamba kuna ulinganifu wa midhihiriko na matumizi ya kiambishi “ka” na “ku” katika lahaja ya Kipemba, katika miundo na maumbo ya maneno. Midhihiriko hio ilibainika katika njeo, mafumbo, nafsi, viambo na tungo masharti. Utafiti uligundua mfanano na tofauti kimaumbo na kimaana baina ya viambishi vya lahaja ya Kipemba na Kiswahili Sanifu. Pia utafiti ulibaini kuwa kiambishi “ka” na “ku” kina mawanda mapana ya matumizi katika lahaja ya Kipemba kikilinganishwa na kiambishi katika Kiswahili Sanifu. Mambo kadhaa yalipendekewza kwa tafiti zijazo zitupie jicho na kuyafanyia kazi. Miongoni mwa mapendekezo hayo ni pamoja na kufanya tafiti linganishi juu ya vilahaja vya Kipemba hasa, kuandikia kazi za viambishi katika vilahaja vidogo vidogo vilivyomo katika kisiwa cha Pemba.
Actions (login required)
|
View Item |