Kuchunguza Uhalisiajabu na Dhamira katika riwaya za Kusadikika na Adili na Nduguze

Abdallah, Zuhura Ali (2019) Kuchunguza Uhalisiajabu na Dhamira katika riwaya za Kusadikika na Adili na Nduguze. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASNIFU YA ZUHURA ALI ABDALLA.pdf] PDF
Download (532kB)

Abstract

Utafiti huu unahusu Kuchunguza Uhalisiajabu na Dhamira katika riwaya za Kusadikika na Adili na Nduguze. Lengo kuu ni “Kuchunguza Uhalisiajabu na Dhamira katika Kusadikika na Adili na Nduguze.” Riwaya hizi ziliandikwa na Shaaban Robert. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Uhalisiajabu kwa lengo la kwanza na swali la kwanza la utafiti. Nadharia ya Mwitiko wa Msomaji imetumika kwa lengo la pili na swali la pili la utafiti huu. Mbinu iliyotumika kukusanyia data ilikuwa ni mbinu ya Usomaji Makini mbapo mtafiti alizisoma kwa kina riwaya teule huku akidondoa data ambazo hatimae zilijibu maswali ya utafiti huu. Data za utafiti huu zilichambuliwa na kuwasilishwa kwa mkabala wa kimaelezo na kitakwimu. Kwa ujumla utafiti huu uliongozwa na malengo mawili na maswali mawili ya utafiti. Lengo la kwanza lilikuwa: Kubainisha vipengele vya uhalisiajabu katika riwaya ya Kusadikika na Adili na Nduguze. Lengo hilo limekwenda sambamba na swali la kwanza la utafiti lisemalo: Ni Vipengele vipi vya Uhalisiajabu vilivyobainishwa katika riwaya ya Kusadikika na Adili na Nduguze?Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa riwaya teule zimetumia vipengele vya uhalisiajabu kama vile; utatizaji wa wakati, masimulizi ya kihalisiajabu, usawiri wa wahusika wa kihalisiajabu, motifu za safari za kihalisiajabu, mitindo ya uumbuzi na udenguzi, na mandhari ya kihalisiajabu. Lengo la pili la utafiti huu lilikuwa: Kubainisha dhamira za uhalisiajabu katika riwaya ya Kusadikika na Adili na Nduguze. Lengo hilo limewiana na swali la pili la utafiti huu lisemalo: Ni dhamira zipi za uhalisiajabu zilizobainishwa katika riwaya ya Kusadikika na Adili na Nduguze? Matokeo ya utafiti huu yamedhihirisha dhamira mbalimbali za uhalisiajabu kama ifuatavyo: Umuhimu wa sheria, uongozi mbaya, ukweli, ukombozi, umuhimu wa huduma za kijamii, ulafi, wivu na choyo. Riwaya ya Adili na Nduguze imebainisha dhamira za: Usaliti, migongano ya mifumo ya kiuchumi ulimwenguni, ukoloni, ukweli, uongozi bora na utabaka.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 800 Literature > 800 Literature, rhetoric & criticism
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr. Administrator OUT
Date Deposited: 21 Sep 2021 08:47
Last Modified: 21 Sep 2021 08:47
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2899

Actions (login required)

View Item View Item